Septemba 13, saa 3:18 usiku, China ilifanikiwa kurusha satelaiti ya "Zhongxing 1E" angani kwa kutumia roketi ya Long March 7 kutoka kwenye Kituo cha Kurushia Satelaiti cha Wenchang. Satelaiti hiyo hutumiwa zaidi kuwapa watumiaji huduma bora za simu, data, redio na televisheni.