Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mamlaka ya afya nchini China imethibitisha visa vipya 62 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, ambapo janga hilo lilizuka mwezi Desemba mwaka jana.
Siku moja kabla watu 32 waliambukizwa virusi vya Corona, kwamujibu wa mamlaka ya afya.
Vifo viwili vya nyongeza vinavyohusiana na COVID-19 vimeripotiwa, Tume ya kitaifa ya afya imesema katika mkutano wake la kila siku na waandishi wa habari.
Kulingana na ripoti ya tume hiyo, visa 81,802 vya maambukizi na vifo 3,333 vimeripotiwa nchini China Bara tangu kuzuka kwa janga hilo.
Wakati huo huo rais Donald Trump amelishukia shirika la afya duniani WHO na kulilaumu kwa kuegemea upande wa China.Trump amesema asasi hiyo ya kimataifa ilishirikiana na China kuficha ukweli kuhusu ugonjwa hatari wa Covid-1.
Rais wa Marekani Trump ametishia kulikatia fedha shirika la afya Duniani WHO kwa sababu amesema shirika hilo halikutilia maanani kwa namna ilivyopasa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona