China yarusha chombo cha anga za juu kumalizia ujenzi wa kituo cha anga za juu cha China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
图像_2022-06-06_141524927.png

China jana imerusha chombo cha anga za juu cha Shenzhou-14 kilichobeba wanaanga watatu watakaomalizia ujenzi wa kituo cha anga za juu cha China katika jukumu litakalochukua miezi sita.

Wanaanga hao watashirikiana na timu iliyoko duniani kumaliza kuunga na ujenzi wa kituo cha anga za juu cha Tiangong, wakikiendeleza kutoka muundo wake wa jengo moja na kukibadilisha kuwa maabara ya kitaifa ya anga za juu yenye maeneo matatu: chombo kikuu cha Tianhe na maabara mbili za Wentian na Mengtian.

Hii ni safari ya 23 ya anga za juu tangu kuidhinishwa na kuanzishwa kwa mradi wa taifa wa anga za juu, na pia ni mradi wa tatu unaohusisha kupeleka wanaanga katika kituo cha anga za juu cha China.
 
Pongezi kwao [emoji122][emoji122]
 
Kwahiyo wanaenda na chakula cha kutengeneza au wanapika uko uko angani
 
View attachment 2251866

China jana imerusha chombo cha anga za juu cha Shenzhou-14 kilichobeba wanaanga watatu watakaomalizia ujenzi wa kituo cha anga za juu cha China katika jukumu litakalochukua miezi sita.

Wanaanga hao watashirikiana na timu iliyoko duniani kumaliza kuunga na ujenzi wa kituo cha anga za juu cha Tiangong, wakikiendeleza kutoka muundo wake wa jengo moja na kukibadilisha kuwa maabara ya kitaifa ya anga za juu yenye maeneo matatu: chombo kikuu cha Tianhe na maabara mbili za Wentian na Mengtian.

Hii ni safari ya 23 ya anga za juu tangu kuidhinishwa na kuanzishwa kwa mradi wa taifa wa anga za juu, na pia ni mradi wa tatu unaohusisha kupeleka wanaanga katika kituo cha anga za juu cha China.
Shenzhou 14🚀
 
Sisi tumerusha mbele tarehe ya uzinduzi safari za SGR
 
Sisi bado tupo kwenye ujima tunaendelea kutumia jembe la mkono
 
Back
Top Bottom