Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
China imesema leo kuwa itapunguza ushuru kuanzia Januari mosi kwenye zaidi ya bidhaa 850 za kigeni ikiwemo nyama ya kuhifadhiwa ya nguruwe, madawa ya maradhi ya pumu na baadhi ya vifaa vya teknolojia ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Tangazo hilo linafuatia makubaliano ya muda ya kibiashara na Marekani katika vita vya ushuru wa bidhaa ambavyo vimeyayumbisha masoko ya kifedha.
Hatua hiyo inaongeza kwa mfululizo wa mapunguzo ya kodi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ambayo serikali ya China inasema yanalenga kuimarisha usambazaji wa bidhaa mbalimbali na kuhimiza ushindani.
Maafisa wa China wanasema hatua hizo hazipaswi kuchukuliwa kama kusalimu amri kwa shinikizo la Marekani