ChinaTech: Kutana na "Rocket Boy" dogo Mchina wa miaka 11 aliyetengeneza rocket. Wazazi jifunzeni kitu hapa.

ChinaTech: Kutana na "Rocket Boy" dogo Mchina wa miaka 11 aliyetengeneza rocket. Wazazi jifunzeni kitu hapa.

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Yan Hongsen mwenye umri wa miaka 11 tu kutoka nchini China aliyepewa jina la utani "Rocket boy" amekuwa gumzo katika mitandao na vyombo vya habari duniani.

Hii ni kufuatia kuweza kutengeneza na kurusha rocket yake ndogo ya kwanza huku followers wake wakitazama tukio hilo kupitia mtandao wa kijamii wa WeiBo.

Yan Hongsen aliwezaje jambo hilo tena akiwa na umri mdogo?

Dogo akiwa kindergarten alianza kuvutiwa na mambo ya Rocket siku baba yake alipompeleka kwenye kituo cha kurushia rocket.
  • Hapa kuna jambo la kujifunza wazazi sio kila siku mtoto unampeleka kubembea na kula ice-cream mpeleke maeneo mengine yatakayoifungua akili yake zaidi.

Yan akavutiwa sana alipojionea jinsi rocket zinavyoruka kwenda angani. Alichojionea siku hiyo kikamfanya aanze kuwa na passion for rockets na astronomy.

Baba yake anasema hapo ndipo mwanaye akaanza kujifunza mwenyewe kwa kina kuhusu mambo ya rocket na astronomy.

Akiwa bado kindergarten "Rocket Boy" alianza kwa kusoma na kujifunza mwenyewe online programming, physics, chemistry, aerospace theory, electronic circuitry, alisoma vitabu, alitazama video na kusoma online forums mbalimbali za astronaouts. Do your kids always only watch cartoons or fictional shows?

Baba yake alipoona jitihada na bidii ya mwanae akampa support kubwa. Kwanza wakaifanya sebule ya nyumbani kwao kama rocket research studio ili dogo awe huru na mambo yake ya rocket science. Je, unafahamu passion au kipaji cha mwanao? Mpe support.

“Sielewi mambo ya vyombo vya angani lakini nitaandamana na mwanangu siku zote. Kama wazazi, tunaunga mkono ndoto za mtoto wetu kikamilifu. Iwapo atakumbana na matatizo ya kiufundi ambayo hawezi kuyatatua, huwasiliana nami kila mara, na mimi hujitahidi niwezavyo kuwasiliana na wataalamu ili kupata usaidizi."
– Baba yake Yan

Rocket yake ya kwanza ilifeli kidogo kwenye parachute malfunction. What to do when your kid feels like a failure?

Lakini baba yake alimtia moyo akamfanya dogo awe calm na kutambua the cause of the failure.

Hilo limemfanya dogo azidi kuboresha pale alipokosea. Na sasa ameshaandika lines codes 600 za flight control system ili kutengeneza rocket yake ya pili anayotazamia kui-launch hivi karibuni.

Alifanikiwa kutengeneza rocket yake ya kwanza ndani ya miezi 10.


View: https://youtu.be/BBw-wzAKqq8?feature=shared


View: https://youtu.be/ZBw5lc7UEaw?feature=shared


Wakati watoto wa Marekani wakifundishwa shuleni kuwa kuna jinsia zaidi ya mbili mambo ni tofauti kwa China.

The future of China technology is in safe hands
 
images (30).jpeg
8b481c87-a33c-4446-a2e8-9abce24f5200_cfe39019.jpg

4e6854ba-3dce-4ba5-a263-f03abe329e47_09e5f8f7.jpg
 
Mtoa post,intelligence like that is not a product of good nurturing,it is innate
Of course it's an incredible innate talent

But this boy's talent is a great example of what can happen when you combine passion with innovation plus good nurturing
 
Kuna vitoto vya buza vimeanza kuunda bomu...tuvipe sapoti
Talents kama hizo zilitakiwa ziwezeshwe kwanza support kutoka ngazi ya familia na serikali

Huyo dogo "Rocket boy" tayari serikali imeshamtambua kama rocket engineer ili kumpa motivation

Na ameruhusiwa kuwapigia pindi hadi wanafunzi wenzake shuleni jinsi ya kutengeneza rocket. Maana yake hapo anatransfer technical know how kwa wenzake

Serikali za wenzetu zinajua jinsi ya kuwaendeleza watoto wenye talent
 
Back
Top Bottom