Chini ya 20% Ya watanzania ndio walipa Kodi

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
• Hapa Ni Ile Kodi ya moja kwa moja
•Kwa takwimu za mwaka Jana Ni 16% ya Nguvu kazi ambayo ndiyo inalipa Kodi Yani Kati ya Nguvu kazi ya Tanzania 33,000,000 Ni watu chini ya milioni nne Pelee ndio wanalipa Kodi
Kama ndivyo nilazima Hawa wachache wanaolipa waione mzigo kwa manufaa ya watu milioni 58 wanaobaki . Hawa watu milioni nne wanaolipa Kodi ya moja kwa moja Mungu awatie nguvu

Kwa mujibu wa habari leo"imesema hadi kufikia Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.

Futeni na hii
 
Kila mtu kulipa Kodi moja kwa moja haiwezekani.. Na kusema kuwa watanzania hawalipi Kodi ni kutotutendea haki.. Kila anayenunua bidhaa dukani huyo ni mlipa Kodi.. Kumbuka kuwa wafanyabiashara wote Kodi wanazolipa huwa wanazijumuisha kwenye bei za bidhaa zao kwa wateja wao.. Kwa hiyo hapa mlipa Kodi mkubwa ni mteja wa mwisho na wala sio huyu anayekusanya na kuzipeleka TRA,..
 
Uko sahihi

Ila naona mleta uzi amezungumzia direct tax na sio indirect kama hiyo ya VAT unayozungumzia

Ila maelezo yako mengine yote uko sahihi na nakuunga mkono
 
Uko sahihi

Ila naona mleta uzi amezungumzia direct tax na sio indirect kama hiyo ya VAT unayozungumzia

Ila maelezo yako mengine yote uko sahih na nakuunga mkono
Kwa mifumo yetu ya uchumi ni ngumu sana kuwa na Walipa Kodi wengi wa moja kwa moja.. Hii ni kwa sababu shughuli nyingi za uchumi sio rasmi.. Na hakuna utaratibu wa makundi haya kulipia Kodi vipato vyao..
 
Ili makudanyo yaongezeke nafikiri tungeanza na kupambana kuwe nashughuli nyingi rasmi za kiuchumi tupate angalau watanzania milioni 20 wanaolipa direct tax. Kati ya milion 33,000,000 Hawa Milion 13 watasaidia kwenye indirect hao wanaobaki Kama milioni 30 niwatoto wadogo under 15 na Wazee wetu over 65
 
Safi kabisa..Kabla ya kufikiria kukusanya Kodi basi tutengeneze walipa Kodi .
 
Yani Kati ya Nguvu kazi ya Tanzania 33,000,000 Ni watu chini ya milioni nne Pelee ndio wanalipa Kodi
Idadi ya walipa Kodi milioni 4 imepatikana kwa kuangalia jumla ya wenye TIN number. Na kama mjuavyo hata bodaboda na bajaji zina TIN number.
 
Je hiyo 16% ni pamoja na wafanyakazi?
Kama ndio, je ikiwa kama mfanyakazi analipa kupitia biashara si 'double' counting?
Kama jibu ni hapana, je wafanyakazi si walipa kodi wa nchi hii?
 
Kila mtu kulipa Kodi moja kwa moja haiwezekani.. Na kusema kuwa watanzania hawalipi Kodi ni kutotutendea haki.. Kila anayenunua bidhaa dukani huyo ni mlipa Kodi.. Kumbuka kuwa wafanyabiashara wote Kodi wanazolipa huwa wanazijumuisha kwenye bei za bidhaa zao kwa wateja wao.. Kwa hiyo hapa mlipa Kodi mkubwa ni mteja wa mwisho na wala sio huyu anayekusanya na kuzipeleka TRA,..
Ni kweli kabisa ndiyo maana nawashangaa wenzangu wauzaji kulalamika kodi sababu anayelipa kodi ni mnunuzi. Wanachofanya ni kuweka bei ya mtaji pamoja na garama za undeshaji biashara faida na kodi ndiyo wanakuja pata bei ya kuuzia. Hiyo ya kusema direct sijui idirect tax ni kama mambo ya kuzunguka mbuyu tu. Mana yake kuna ile kodi ambayo unaiona moja kwa moja umekatwa mfano wafanyakazi ile ni direct ila huku tunaponunua soda beer sijui sigara unakutana na bei tu kumbe ndani tayari kuna kodi. Hakuna mfanyabiashara anayelipa kodi zote zinakuwa adjusted kwenye bei ya bidhaa. Ndiyo maana kodi ya beer ikipanda na bei ya beer utasikia imepanda. St Paka Mweusi umesema ukweli japo ni mchungu watu watakuja na povu ila ndiyo ukweli wenyewe.
 
Je hiyo 16% ni pamoja na wafanyakazi?
Kama ndio, je ikiwa kama mfanyakazi analipa kupitia biashara si 'double' counting?
Kama jibu ni hapana, je wafanyakazi si walipa kodi wa nchi hii?
Akiwa mfanyakazi anakatwa kwenye personal income tax, PAYE

Na akiwa kwenye biashara atalipa direct tax kulingana na category aliyopo

Kwa hiyo hapo hakuna double counting
 
Ulishawahi kufanya biashara?

Back
Top Bottom