St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,956
- 5,149
Hapa wafanyabiashara wanakuwa wabishi TU.. Lakini huu ndio uhalisia.. Kile anachokiuza kwa mteja wake anaweka hapo mtaji wake, usalfirishaji, Kodi na faida yake..Ni kweli kabisa ndiyo maana nawashangaa wenzangu wauzaji kulalamika kodi sababu anayelipa kodi ni mnunuzi. Wanachofanya ni kuweka bei ya mtaji pamoja na garama za undeshaji biashara faida na kodi ndiyo wanakuja pata bei ya kuuzia. Hiyo ya kusema direct sijui idirect tax ni kama mambo ya kuzunguka mbuyu tu. Mana yake kuna ile kodi ambayo unaiona moja kwa moja umekatwa mfano wafanyakazi ile ni direct ila huku tunaponunua soda beer sijui sigara unakutana na bei tu kumbe ndani tayari kuna kodi. Hakuna mfanyabiashara anayelipa kodi zote zinakuwa adjusted kwenye bei ya bidhaa. Ndiyo maana kodi ya beer ikipanda na bei ya beer utasikia imepanda. St Paka Mweusi umesema ukweli japo ni mchungu watu watakuja na povu ila ndiyo ukweli wenyewe.
Ndio maana Bei ya mafuta ikipanda bei za bidhaa zinapanda.. Kodi ikipanda bidhaa zinapanda bei pia..
Hapa mfanyabiashara anasimama kama mkusanyaji wa Kodi na kuwakilisha TRA..