Chini ya 20% Ya watanzania ndio walipa Kodi

Hapa wafanyabiashara wanakuwa wabishi TU.. Lakini huu ndio uhalisia.. Kile anachokiuza kwa mteja wake anaweka hapo mtaji wake, usalfirishaji, Kodi na faida yake..

Ndio maana Bei ya mafuta ikipanda bei za bidhaa zinapanda.. Kodi ikipanda bidhaa zinapanda bei pia..

Hapa mfanyabiashara anasimama kama mkusanyaji wa Kodi na kuwakilisha TRA..
 
Ni kweli kabisa ndiyo maana nawashangaa wenzangu wauzaji kulalamika kodi sababu anayelipa kodi ni mnunuzi
Indirect tax kama hiyo VAT ni njia ya serikali kumtumia mfanyabiashara kukusanya kodi kutoka kwa mnunuaji wa mwisho wa bidhaa kwa hiyo mfanyabiashara haathiriki na VAT

Ila naye mfanyabiashara lazima alipe kodi sasa hapo ndipo anapokutana na direct tax kutoka kwenye faida yake ya mauzo. Hii lazima apambane mwenyewe
 
Magu akuwa mjinga kutoa vitambulisho vya watu wenye mitaji chini ya million 4 hadi shillingi Moja sasa hivi hao watu wote awalipi chochote Kwa kiasi kikubwa nenda vijijini Kuna maduka , migahawa n.k wanafanya biashara na awachangii chochote serikalini.
 
Inaonekana hujui lolote kuhusu biashara, Mfanyabiashara analipa kodi kwenye faida yake inayobaki baada ya kuuza. Kama ni kampuni ni 30% kama ni individual haitofautoani sana na PAYE. Sasa hiyo kodi anakupaje mtu wa mwisho na akishauza ndo kodi inakokotolewa?
 
TRA anakusanya kodi zake alizomlenga raia wa kawaida kupitia mfanyabiashara na kwa gharama za mfanyabiashara AND STILL MFANYABIASHARA ANALIPA KODI YAKE KAMA KAWAIDA.
 
Hivi karibuni TRA inakuja kitu kinaitwa TAX Retun forms, naona Mwigulu leo kaanza kwa mbali, aliposema sasa kodi zinazohusiana na majengo zitasghughulikiwa na kuanza kulipwa kwenye ngazi ya mtaa. Nikaona "hayooooo yamefika".

Huo ndiyo mwanzo wa kila raia kuanza kujaza forms za TAX Returns kama Marekani. Hapo ndipo tutakapoanzia raia wpte wa umri wa kulipa kodi kulipa kodi, kwani kila raia itaboidi ajaze form kila mwaka kuonesha alipozipata pesa anazotumia.

Jitayarisheni kisaikolojia, hamtaki kustuliwa mkapata ugonjwa wa moyo. Sijui nauza vitumbua, nauza mbege, nalima mboga, nauza gongo ndiyo hustahiki kulipa kodi imepitwa na wakati. Hesabu zijionesha zenyewe ukijaza form, kipato na magtumizi yako ndiyo yataamua.

Kuanzia JULY anzeni kuj9tayarisha kuwapokea Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Mtendaji na afiusa wa kodi, watawapa elimu ya kutosha na urafiki kabisa kwa kuanzia na kodi ya jengo, watakufanya ujione upo sslama kabisa, kwa kuwa wanataka data zako.

Tutalipa tu wote tunaostahiki kulipa kodi za moja kwa moja.

Pia ipelekee tunapokosa za kulipa tunalipwa sisi, kwani serikali itakusanya pesa nyingi sana, mara hata 100 zaidi ya makusanyo ya sasa kwa mwaka.
 
Pia 80% hawategemei mshahara ktk kuendeleza maisha yao, ajabu hao ambao ni chini ya 20% hua wanadhani ndo wanayo thamani kuliko hawa 80% ktk taifa hili la tz

20% waliamua hatima ya jpm ingawa 80% walimhitaji kwa kila hali
 
Mleta mara akili huna hujui kana hata kusoma takwimu za sensa kuwa Asilimia 80 ya wanzania wanaishi vijijini Kwa subsistence economy lakini Kodi wanalipa vizuri tu kupitia indirect tax
Kodi wanalipa kupitia bidhaa wananunua Zina tax ndani na vocha wanaweka kwenye simu na umeme wa nyumba zao

Pumbavu kiafisa kibarua mwajiriwa serikalini wewe
Gesi ukinunua ya kupikia Kodi ipo
Tiketi ya basi au treni ukinunua Kodi ipo Unaposema Kodi hawalipi walioko kwenye subsistence economy unamaanisha Nini! Kwani Kodi lazima iwe income tax tu ndio umtambue mtu kuwa mlipa Kodi?

Hizo data za kusema wachache tu Asilimia 20 umezitoa wapi Wakati hata vocha ukiweka ya simu Kodi imo
 
Newbies umeishia la ngapi wewe? Unazungumzia kodi? Kuna kodi aina ngapi?
Ngoja nikupe somo hapa wala sitokudai ada..
Kuna kodi aina mbili...
Kodi ya moja kwa moja(direct) na isiyo ya moja kwa moja(indirect)..

Indirect hulipwa na 100% ya watanzania.Ukinunua vocha, sukari etc unalipa kodi...

Kwa kusema chini ya 20% wanazungumzia direct, na hii kodi hulipwa na wafanyakazi au wafanyabiashara... kabla hujaja kupost kitu hapa kusema <20% hulipa kodi.. jiulize basi waajiriwa plus biashara tz ni <20%. Kisha jiulize kwanini?

Kwasababu
a) hakuna ajira nchini... kama hamna ajira unategemea walipakodi watoke wapi?
b)waajiriwa(wanasiasa) wenu hawalipi kodi. Ulizia rais,wabunge analipa kiasi gani cha kodi?

Chakufanyika..
Serikali iwezeshe mazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji... nani afungue kampuni tz? Yaani 50% kodi za serikali, 50% ugawe faida, mtaji etc...
Lipa atleast 5000 umeme mwanzoni mwa mwezi utanambia... from 5000 unaoneshwa umelipa 2700.. so 2300 ni kodi... ni lini unadhani mwenye akili timamu atawekeza huku???????
 
Wanaolipa kodi kihalali ni nduguzangu waalimu, wauguzi, madaktari, matarishi nk ambao wanakatwa PAYE.
Waliobaki kina mangi na mamilionea ni magumashi tu
 
RRu
Rudia kusoma nilichoandika Kisha u comment tena
 
Umeelewa nilichoandika?
 
hizo ni nyimbo nyimbo, malengo yao nu kutuzidishia mzigo wa makodi tu, wanajaribu kubipubipu
 
Nitatizo kwa nchi yetu . Juhudi zifanywe kuongeza idadi ya walipa kodi
 
Je hiyo 16% ni pamoja na wafanyakazi?
Kama ndio, je ikiwa kama mfanyakazi analipa kupitia biashara si 'double' counting?
Kama jibu ni hapana, je wafanyakazi si walipa kodi wa nchi hii?
Hata Hilo kundi lipo humo humo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…