Chini Ya kapeti, Nyoni hakuwa na kadi 3 njano

Hilo halina ubishi mkuu. Huyo anatafuta sababu baada ya wamatopeni kuangukia pua kwa miaka kadhaa sasa. Shabiki wa mpira huwezi kuacha timu yako hata ikishuka daraja.
Swadakta maneno yako ndo maana nikamjibu namna hiyo.
 
Pale uwanjani kuna waamuzi zaidi ya watatu na hutoa taarifa zote za LAZIMA kila baada ya mchezo kumalizika. Sasa hizo CD za nini?
 
Kwani tff hawana mikanda yao? Na je report za waamuzi hazihifadhiwi? Kuna haja ya TFF kuajiri mweka kumbukumbu kwa hard copy na soft copy au electronic
 
Ligi ya bongo inaendeshwa kwa majungu tu....na bingwa anapatikana kwa majungu na kununua nunua mechi na ujanja ujanja mwingine.......
 
Kwani tff hawana mikanda yao? Na je report za waamuzi hazihifadhiwi? Kuna haja ya TFF kuajiri mweka kumbukumbu kwa hard copy na soft copy au electronic
1. Best Practice: Kila mdau anaweka kumbukumbu ya kadi kwa wachezaji wa kila timu: timu zenyewe, vyombo vya habari, chama cha mpira nk. Katika mazingira haya ambayo kila mechi inaoneshwa live, huwa hakuna kadi inayoonekana na washabiki wa kiwanja au timu moja tu. Hadhira yote inayoshuhudia mechi husika inajua, huku vyombo vya habari vinavyoonesha au kutangaza mechi hiyo ikionesha mjumuiko wa kadi za kila mchezaji. Ndiyo maana hata bila ya kuwasiliana na FA au waendeshaji mashindano, vyombo hivyo vya habari vinatangaza Mara moja mchezaji anapotimiza kadi inayomweka nje kwenye mechi zinazofuata. Hakuna kinachofanyika nyuma ya pazia. Vyombo vinavyopewa haki ya kuonesha/kutangaza mashindano husika huwa havina maslahi (interests) na timu yoyote inayoshiriki.
2. Good Practice: Kila mdau anaweka kumbukumbu ya kadi kwa wachezaji wake. Lakini kwa sababu michezo yenyewe yote haishuhudiwi live muda wote, chama cha mpira kitakuwa ndio mamlaka kuu ya takwimu hizo. Kwenye kila Kikao cha kabla ya mechi (pre-match meeting) chama cha mpira kitazitahadharisha timu husika iwapo kuna mchezaji hastahiki kucheza mechi inayojadiliwa kutokana na kukusanya idadi ya kadi iliyowekwa na kanuni. Kama kuna kuhitilafiana baina ya FA hiyo na timu husika kuhusu idadi ya kadi, timu husika inaweza kumchezesha mchezaji huyo kwa kubahatisha (at their own risk) na baadaye kufananisha takwimu zao, za wadau wengine na za FA. Wanaweza kufanya hivyo wakijua kwamba hata kama watashindwa rufaa kwa kuwa takwimu za FA ndio rasmi zaidi, bado wana nafasi ya kukata rufaa kwenye mamlaka husika ambazo zinaweza kuhoji usahihi wa takwimu za FA.
3. Worst Case Scenario: Ni FA tu ndiyo yenye mamlaka ya kuweka takwimu za kadi, FA ambayo haiitahadharishi timu yenye mchezaji anayeziwilika kwa kuwa na kadi nyingi, haitoi ushindi wa moja kwa moja pale mchezaji wa aina hiyo anapocheza mechi hiyo mpaka timu pinzani ikate rufaa, vyombo vya habari vinavyoweza kufuatilia na kutahadharisha timu husika isimchezeshe mchezaji mwenye kadi havifanyi hivyo kwa sababu vyenyewe vina maslahi kwenye baadhi ya timu washiriki.
 
Ulisema kweli. Azam wamekata rufaa na sie tumeshafikisha pt 71 saafi.
 
Hitimisha sasa hoja zako. Je Nyoni alikuwa na kadi tatu?
 
Hitimisha sasa hoja zako. Je Nyoni alikuwa na kadi tatu?
Nilivyo ndivyo ulivyo, ndivyo alivyo kila mdau kwa sababu hakuna uwazi katika kuweka takwimu za kadi. Atavyosema TFF ndiyo hivyohivyo. Ndiyo worst case scenario niliyoifafanua awali.
 
Ligi ya bongo inaendeshwa kwa majungu tu....na bingwa anapatikana kwa majungu na kununua nunua mechi na ujanja ujanja mwingine.......
kwani simba nae alimuuzia yanga mechi?acheni mawazo mgando kocha mayanja amesema facts kuwa kilichoikwamisha simba Ni ufinyu WA kikosi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…