Kete Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 6,656
- 6,886
Shida sio timu kiongozi shida ni uongozi wa soka lenyewe, uongozi awamu hii umefeli vibaya, figisufigisu kila uchao.Mshabiki wa kweli haachi hata kama timu yake iko mchangani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shida sio timu kiongozi shida ni uongozi wa soka lenyewe, uongozi awamu hii umefeli vibaya, figisufigisu kila uchao.Mshabiki wa kweli haachi hata kama timu yake iko mchangani.
Swadakta maneno yako ndo maana nikamjibu namna hiyo.Hilo halina ubishi mkuu. Huyo anatafuta sababu baada ya wamatopeni kuangukia pua kwa miaka kadhaa sasa. Shabiki wa mpira huwezi kuacha timu yako hata ikishuka daraja.
Pale uwanjani kuna waamuzi zaidi ya watatu na hutoa taarifa zote za LAZIMA kila baada ya mchezo kumalizika. Sasa hizo CD za nini?Taarifa zilizopo ni kwamba Azam wamepeleka barua tff ya kupitia tena michezo ya azam ili kujiridhisha kama kweli alikuwa na kadi 3 za njano. Pia wamepeleka cd zote za michezo ya azam,
Hapa yanga anapaswa kushinda Game ya Jumanne dhidi ya Mbeya city ili kujihakikishia ubingwa, Maanake hawa tff hawaeleweki.
Wewe ni simba tu, huna jipyaHivi kunawenye akili timamu anashabikia mpira wa Tz ?!!?? Mpk leo
Kama yupo huyo ni jasili
Kwani tff hawana mikanda yao? Na je report za waamuzi hazihifadhiwi? Kuna haja ya TFF kuajiri mweka kumbukumbu kwa hard copy na soft copy au electronicH
Hapa ndipo inapokuja hoja yangu ya ukakasi wa Azam TV kupewa haki za kurusha matangazo ya Ligi ambayo timu ya kampuni yao mwenza inacheza. Ndio mgongano wa kimaslahi ambao nimekuwa nikiitetea Yanga kwenye msimamo wao wa kukataa hilo (ingawa wao wameliangalia kipesa zaidi). Angalia sasa: (1) Azam TV watakuwa waungwana kiasi gani kuonesha matokeo yatayoiumiza Azam FC kwenye video hizo? (2) Hata uungwana huo ukiwapo, Mbeya City watakuwa na imani gani kwamba Azam TV haikuchezea mikanda hiyo ili kufuta matukio ya Nyoni kuoneshwa kadi nyekundu? (3) Kwa mfano Azam TV watashinda rufaa yao kwa mgongo wa video za Azam TV, mamlaka za rufaa zitachukua sekunde ngapi kuipa ushindi Mbeya City itapotumia ukweli huo wa mgongano wa kimaslahi wa Azam TV na Azam FC?
Tujifunze. Ukupigao ndio ukufunzao!
Sasa hapa unaharibu mkuu. Ukishindwa kubali kushindwa urekebishe makosa yako, msimu ujao uwe fitiLigi ya bongo inaendeshwa kwa majungu tu....na bingwa anapatikana kwa majungu na kununua nunua mechi na ujanja ujanja mwingine.......
Timu yenu si ijipange tuu, sasa ligi ina kosa gan hapoLigi ya bongo inaendeshwa kwa majungu tu....na bingwa anapatikana kwa majungu na kununua nunua mechi na ujanja ujanja mwingine.......
1. Best Practice: Kila mdau anaweka kumbukumbu ya kadi kwa wachezaji wa kila timu: timu zenyewe, vyombo vya habari, chama cha mpira nk. Katika mazingira haya ambayo kila mechi inaoneshwa live, huwa hakuna kadi inayoonekana na washabiki wa kiwanja au timu moja tu. Hadhira yote inayoshuhudia mechi husika inajua, huku vyombo vya habari vinavyoonesha au kutangaza mechi hiyo ikionesha mjumuiko wa kadi za kila mchezaji. Ndiyo maana hata bila ya kuwasiliana na FA au waendeshaji mashindano, vyombo hivyo vya habari vinatangaza Mara moja mchezaji anapotimiza kadi inayomweka nje kwenye mechi zinazofuata. Hakuna kinachofanyika nyuma ya pazia. Vyombo vinavyopewa haki ya kuonesha/kutangaza mashindano husika huwa havina maslahi (interests) na timu yoyote inayoshiriki.Kwani tff hawana mikanda yao? Na je report za waamuzi hazihifadhiwi? Kuna haja ya TFF kuajiri mweka kumbukumbu kwa hard copy na soft copy au electronic
Ulisema kweli. Azam wamekata rufaa na sie tumeshafikisha pt 71 saafi.Hadithi imegeuka tena .... Nyoni hakuwa na kadi tatu za njano?! ..Ngoja kwanza nimuombe Mungu azidi kunipa uhai na Movie hii katika soka la bongo nione inaishiaje!!!!!!!!??? Mtanielewa .
Walevi wanasema raha ya pombe unywe ulewe na sio kushiba au kujaza tumbo ndiii. Likithibitika hili ni kweli na Azam kurudishiwa alama zake tatu basi si vibaya hizo ofisi mkawaachia na wengine . No matter what tumejipanga na huu ubingwa.
Ilivyo sasa Azam akishinda mechi zote anakuwana 66 akiongezewa na hizi 3 atakuwa na 69. Yanga hivi sasa ana alama 68 na mechi tatu mkononi ambazo itamuhitaji alama 3 tu kuachana na mashaka haya . Hii itamfanya Yanga afikishe 72 !. Simba akimaliza zote ni 67!!.
Hitimisha sasa hoja zako. Je Nyoni alikuwa na kadi tatu?1. Best Practice: Kila mdau anaweka kumbukumbu ya kadi kwa wachezaji wa kila timu: timu zenyewe, vyombo vya habari, chama cha mpira nk. Katika mazingira haya ambayo kila mechi inaoneshwa live, huwa hakuna kadi inayoonekana na washabiki wa kiwanja au timu moja tu. Hadhira yote inayoshuhudia mechi husika inajua, huku vyombo vya habari vinavyoonesha au kutangaza mechi hiyo ikionesha mjumuiko wa kadi za kila mchezaji. Ndiyo maana hata bila ya kuwasiliana na FA au waendeshaji mashindano, vyombo hivyo vya habari vinatangaza Mara moja mchezaji anapotimiza kadi inayomweka nje kwenye mechi zinazofuata. Hakuna kinachofanyika nyuma ya pazia. Vyombo vinavyopewa haki ya kuonesha/kutangaza mashindano husika huwa havina maslahi (interests) na timu yoyote inayoshiriki.
2. Good Practice: Kila mdau anaweka kumbukumbu ya kadi kwa wachezaji wake. Lakini kwa sababu michezo yenyewe yote haishuhudiwi live muda wote, chama cha mpira kitakuwa ndio mamlaka kuu ya takwimu hizo. Kwenye kila Kikao cha kabla ya mechi (pre-match meeting) chama cha mpira kitazitahadharisha timu husika iwapo kuna mchezaji hastahiki kucheza mechi inayojadiliwa kutokana na kukusanya idadi ya kadi iliyowekwa na kanuni. Kama kuna kuhitilafiana baina ya FA hiyo na timu husika kuhusu idadi ya kadi, timu husika inaweza kumchezesha mchezaji huyo kwa kubahatisha (at their own risk) na baadaye kufananisha takwimu zao, za wadau wengine na za FA. Wanaweza kufanya hivyo wakijua kwamba hata kama watashindwa rufaa kwa kuwa takwimu za FA ndio rasmi zaidi, bado wana nafasi ya kukata rufaa kwenye mamlaka husika ambazo zinaweza kuhoji usahihi wa takwimu za FA.
3. Worst Case Scenario: Ni FA tu ndiyo yenye mamlaka ya kuweka takwimu za kadi, FA ambayo haiitahadharishi timu yenye mchezaji anayeziwilika kwa kuwa na kadi nyingi, haitoi ushindi wa moja kwa moja pale mchezaji wa aina hiyo anapocheza mechi hiyo mpaka timu pinzani ikate rufaa, vyombo vya habari vinavyoweza kufuatilia na kutahadharisha timu husika isimchezeshe mchezaji mwenye kadi havifanyi hivyo kwa sababu vyenyewe vina maslahi kwenye baadhi ya timu washiriki.
Nilivyo ndivyo ulivyo, ndivyo alivyo kila mdau kwa sababu hakuna uwazi katika kuweka takwimu za kadi. Atavyosema TFF ndiyo hivyohivyo. Ndiyo worst case scenario niliyoifafanua awali.Hitimisha sasa hoja zako. Je Nyoni alikuwa na kadi tatu?
kwani simba nae alimuuzia yanga mechi?acheni mawazo mgando kocha mayanja amesema facts kuwa kilichoikwamisha simba Ni ufinyu WA kikosi,Ligi ya bongo inaendeshwa kwa majungu tu....na bingwa anapatikana kwa majungu na kununua nunua mechi na ujanja ujanja mwingine.......