Haya ni maneno niliyoambiwa na jounalist wa ki Danish alikuja Tanzania baada ya American Embassy kupigwa bony 2008.
Anasema alitokea kupenda kiepe, sasa alikuwa Posta Mpya akaona container enzi zile wanakaanga chips. Kufika pale alijitahidi kuongea kwa mdomo na vidole kuonyesha kuwa anahitaji sahani ya chips.
Wale vijana wauzaji wote walipata woga, walimkwepa mteja anaemwaga ngeli. Kijana mmoja kwa ujasiri alijitokeza na kumuuliza “chips egg far far or confused sir”? Yule kijana akimaanisha kiepe au yai juu.
Yule mzungu aliniambia yule kijana akijiendeleza atafika mbali, alijua technical words za kufikisha ujumbe.