PreGE2025 Chiwelesa: Mradi wa maji wa Nyakanazi kuwa mwarobaini wa tatizo la maji Biharamulo

PreGE2025 Chiwelesa: Mradi wa maji wa Nyakanazi kuwa mwarobaini wa tatizo la maji Biharamulo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
12,213
Reaction score
28,916
RUWASA BIHARAMULO WAANZA KUTEKELEZA KWA KASI MAELEKEZO YA KATIBU MKUU NCHIMBI UJENZI WA MRADI MKUBWA WA MAJI NYAKANAZI, TUNAJENGA MRADI WENYE THAMANI YA BIL 2.9 "TUNATARAJIA KUONDOA KABISA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA ENEO LA NYAKANAZI" - BIHARAMULO.*

📍 Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Maji katika Kijiji Cha Nyakanazi, RUWASA Wilaya ya Biharamulo.

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijinini (RUWASA) imeanza kutekele, a maagizo ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kwa Wizara ya maji aliyoyatoa katika Kijiji Cha Nyakanazi wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya biharamulo, mkoa wa Kagera baada ya wananchi wa eneo Hilo kupitia mwakilishi wao Mhe Eng Ezra Chiwelesa (MP) kuwasilisha kero hiyo ambapo serikali imetoa jumla ya Tshs Bil 2.9 kwaajili ya Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa maji ambao unatarajiwa kuwa suluhisho la ukosefu wa maji katika eneo Hilo.

Akizungumza kuhusu mradi huo Meneja wa RUWASA Wilaya ya Biharamulo Eng Lucas Matina amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa umeanza ambapo mradi huo utakwa na;
1. Ujenzi wa ofisi ya CBWSO
2. Uchimbaji na ulazaji wa Bomba kilomita 44
3. Ujenzi wa Tanki lenye ujazo wa Lita 680,000
4. Ujenzi w tenki lenye ujazo wa Lita 300,000.
5. Ujenzi wa tenki lenye ujazo WA Lita 200,000.
6. Ujenzi wa vituo vya kuchotea Maji Kwa njia ya malipo ya kabla(Card) vituo 10
7. Ununuzi wa mita za malipo ya kabla(luku-kwa ajili ya taasisi za umma) 40.
Kukamilika kwa Mradi huu kutaondoa kabisa Changamoto ya ukosefu wa maji katika vijiji vya Nyakanazi na Nyakafundikwa ambayo ni maeneo yanayokua Kwa Kasi.

"Tunamshukuru sana Mhe Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha kwaajili ya utekelezaji wa mradi huu mkubwa utakaoondoa adha ya maji katika Vijiji vyaa nyakanazi na nyakafundikwa tunaahidi kuwa Tutahakikisha tunafanya kazi mchana na usiku ili mradi huu ukamilike kabla ya wakati ili wananchi waweze kupata huduma ya maji RUWASA tunatambua kuwa maji ni huduma isiyo na mbadala" alisema Eng Lucas Matina
FB_IMG_1748452401050.jpg
FB_IMG_1748452406694.jpg
FB_IMG_1748452412301.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1748452404034.jpg
    FB_IMG_1748452404034.jpg
    51.9 KB · Views: 34
Back
Top Bottom