KWELI Chokaa inaweza kuchangia kuongezeka kwa ubora na ufanisi wa mbolea katika kilimo cha ndizi

KWELI Chokaa inaweza kuchangia kuongezeka kwa ubora na ufanisi wa mbolea katika kilimo cha ndizi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Mdau katika jukwaa la Kilimo, Ufugaji na Uvuvi amehoji kama ni kweli chokaa inachangia ubora na ufanisi wa mbolea katika kilimo cha ndizi?

"Nilikiwa kwenye Mkoa wa Kagera ambapo kuna mwenendo unaoongezeka wa wakulima wa ndizi kutumia chokaa katika mashamba yao. Wakulima hao wanadai kuwa matumizi ya chokaa husaidia migomba kustawi vizuri na kupunguza au kuzuia mashambulizi ya baadhi ya wadudu wanaosababisha kudhoofika au kuharibika kwa migomba." Ameeleza.
1767785316233.png
 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa utafiti 'Impact of Application of Fertilizer and Lime on Yieldof Banana (Grand Naine) and Soil Parameters inAcidic Soil of Arunachal Pradesh' uliofanywa Siang Magharibi nchini India na kuchapishwa katika jarida la kimataifa la Mimiea na Sayansi ya Udongo' (International Journal of Plant & Soil Science) matumizi ya chokaa na mbolea yanachukuliwa kuwa nyenzo muhimu katika kurekebisha udongo wenye asidi katika maeneo ya mid hill ya Arunachal Pradesh nchini India. Matumizi ya chokaa pamoja na mbolea yanapendekezwa ili kuongeza rutuba ya udongo pamoja na mavuno na ubora wa ndizi.

Matokeo ya utafiti huo yanaonesha umuhimu wa matumizi ya chokaa katika kupunguza sumu ya alumini (Al) na kuongeza mkusanyiko wa kalsiamu (Ca), ambayo inajulikana kuwa huchangia kwa kiasi kikubwa ubora wa matunda kwa kuimarisha kuta za seli.

Vilevile inaelezwa kuwa matumizi makubwa ya chokaa pekee hayawezi kuwa njia bora ya kuondoa vikwazo vinavyopunguza ukuaji katika uzalishaji wa ndizi. Inapendekezwa kutumia asilimia 50 ya chokaa (liming) kwa kuunganisha na asilimia 100 ya kiwango cha mbolea kinachopendekezwa (RDF) ili kuongeza mavuno na ubora wa ndizi katika maeneo ya milima.

Tovuti ya Kinsey Agricultural Services inabainisha kuwa kutumia chokaa kwa kiwango kilichopitiliza kutaweza kwa kiasi fulani kupunguza virutubisho vingine muhimu vinavyohitajika na mimea inayopandwa hapo, na mkulima anapaswa kujua ikiwa hali hii ipo kabla ya kutumia kiasi kikubwa cha chokaa.

Utafiti mwingine "The Effectiveness of Chemical Fertilizer Combined with Lime, CowManure and Indigenous Nitrogen-Fixing Bacteria İnoculationon Soil Fertility and White Bean Yield" uliochapishwa katika jarida la Malaysian Journal of Soil Science katika matokeo yake unataja ongezeko la chokaa, iwe kando au kwa mchanganyiko, limeboresha kikamilifu mavuno na ubora wa mimea.

Hivyo unasisitiza kuwa ni muhimu kutumia chokaa, mbolea, pamoja ili kuongeza mavuno na kuboresha ubora wa mazao katika udongo na maji ya umwagiliaji.​
Back
Top Bottom