Chokoleti inavyoweza kukupa bakteria wa homa ya matumbo, watoto wameathirika zaidi

Chokoleti inavyoweza kukupa bakteria wa homa ya matumbo, watoto wameathirika zaidi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Salmonella Typhimurium.jpg

Aprili 27, 2022, Uingereza ilitoa taarifa kwa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) kuhusu kundi la wagonjwa wenye maambukizi ya bakteria wa Salmonella Typhimurium.

Uchunguzi ulihusisha mlipuko huo na chokoleti ambayo imesambazwa katika nchi 113.

Ripoti ya WHO inaeleza zaidi ya watu 150 wamekutwa na Bakteria wa Salmonellosis ikiwemo kutoka Nchi za Ubelgiji, Marekani na Uingereza baada ya kula chokoleti, hali ambayo imefanya watoe tahadhari juu ya ulaji wake hasa kwa watoto ambao ndiyo waathirika wakubwa katika utafiti huo

Bakteria hao wanashambulia tumbo na damu, ndio husababisha Ugonjwa wa Homa ya Matumbo (Typhoid). Watoto chini ya miaka 10 ndio waathirika wakubwa, asilimia 89 ikiwa ni wao ndio waathirika wa magonjwa ya tumbo

Tahadhari ya kimataifa ilitolewa na INFOSAN tarehe Aprili 10, 2022 na kuanzisha mkakati wa kimataifa ya kurejeshwa kwa bidhaa.

Mlipuko katika nchi 113
WHO imeeleza mlipuko huo unahusishwa na bidhaa za Kinder zinazozalishwa Nchini Ubelgiji na ambazo zimesambazwa katika nchi 113.

Ingawa hadi sasa shirika hilo linasema hakujakuwa na vifo vyovyote vilivyosababishwa na mlipuko huo lakini watoto chini ya umri wa miaka mitano ndio wanaoathirika zaidi.

Shirika la Uingereza la Usalama wa Afya lilithibitisha wagonjwa 73, idadi ambayo ni kubwa zaidi ulimwenguni.

Kuna visa vinavyoshukiwa katika nchi 10 zaidi ambazo ni Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Luxemburg, Uholanzi, Norway, Uhispania, Uswisi na Marekani.

Nchini Uingereza, watoto walioambukizwa ni wa chini ya umri wa miaka 10 na asilimia 66% ni wasichana.

Tahadhari ya kimataifa
Shirika hilo la afya duniani linasema moja ya dalili ni kuhara damu.

Baada ya kutolewa tahadhari ya kimataifa, Aprili 10, 2022 kulikuwa na wito wa kuondoa bidhaa hizo kwenye soko.

Hatari ya kuenea kwa mlipuko huo wa Salimonella Ulaya na ulimwengu kote inachukuliwa kuwa ya wastani mpaka kutakapopatikana habari kuhusu idadi ya jumla ya chokoleti zilizotolewa sokoni.

Usugu wa dawa
WHO inasema aina hiyo ya salimonella ni sugu kwa aina sita za antibiotics ambazo ni penicillins, aminoglycosides, phenicols, sulfonamides, trimethoprim, na tetracyclines.

Wale walioambukizwa huugua salmonella baada ya kuambukizwa salmonella serotypes typhimurium na enteritidis.

Ugonjwa huo unaweza kudumu kati ya siku mbili hadi saba.

Dalili zinazoonekana kati ya saa sita na 72 za mwanzo ni pamoja na homa kali, maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kutapika, na kuhara ambazo zinaweza kusababisha kuvuja damu kama inavyoripotiwa katika visa vingi kwenye mlipuko wa sasa.

Chanzo: News.un
 
Duuuuh. Afadhali watoto wangu hawapendi hizi vitu
 
Ni Chocolates zote au Chocolates maalum???

Diary Milk na Snickers hazikosi ndani mwangu.
 
Back
Top Bottom