Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI!
Umri…………………..🔞
Sehemu ya 6
******
Waasema mtaka cha uvunguni sharti ainame,ndicho kilichotokea kangu,stori ya mgeni aliyeleta utata kijijini niliitaka sana,ivyo ilinibidi niwe mpole!
Regina alifanya upuuzi wake akamaliza akaketi kisha akaniangalia usoni akasema
“Sasa nakupa hadithi ya mgeni,ila chonde usinibake maana tupo wawili tu hapa bora baba angekuwepo!”
“Regina bhana nilishakutana na kina chausiku sikuwabaka kina kidawa na mwisho Lisa sembuse huyo mgeni?Nipe stori mimi acha uoga!”
“Sawa napenda watu wanaojiamini kama wewe!”
“Leta mambo!”
*********
Miaka kumi iliyopita kijiji chetu kilimpokea mgeni,mgeni ambaye aliacha majonzi makubwa kijijini,mgeni ambaye ameziba kabisa milango ya wageni kupokelewa katika kijiji chetu!
Ilikuwa usiku kama saa mbili siku hiyo ilikuwa inanyesha mvua kubwa sana,wenye nyumba za bati walikuwa bize wakikinga maji safi ya mvua,maana kama unavyoona kijiji chetu tunatumia maji ya kisimani!
Mzee mmoja maarufu kama mzee Jomo alikuwa ndani na familia yake,wao maji ya mvua yaliwapita sababu hakuwa ameezeka nyumba yake kwa bati!
“Unaona sasa mume wangu tungekuwa na bati tungekuwa tunafaidi maji ya mvua hapa!”,alisema mke wa mzee Jomo!
“Mkewangu wewe subiri yani safari hii nikiuza mpunga wangu najenga nyumba kubwa sana hapa naezeka na vigae kabisa sitaki bati mimi!”
“Baba muogope Mungu na huku ukiuza tu unaoa hapa nyumbani huonekani pesa zote kwenye pombe!”,alisema binti mkubwa kati ya mabinti zake wanne alionao,Mzee Jomo mpaka alipofikia hajabahatika kupata mtoto wa kiume,alishawahi kujaribu kuchepuka akampa mimba mwanamke mwingine lakini napo akapata mtoto wa kike!
“Mwambieni baba yenu!Mi nishamaliza maneno yote na safari hii akiuza mpunga akakimbia hasirudi hapa anakuta nami nimeolewa!”
“Haahhahahahahah mamaaa acaha kutuchekesha!”
Mabinti wa mzee Jomo walicheka kwa pamoja,kauli ya mama yao iliwachekesha sana,Mzee Jomo hakuwa mkali sana kwa familia yake kiasi kwamba hata mabinti zake hawakuwa wanamuogopa kiivyo!
“Mnacheka kwa hiyo mnasapoti upuuzi wa mama yenu ebhu nendeni mkalale!”
Alisema Mzee Jomo mabinti zake wakainuka ila kabla hawajaingia chumbani mlango uligongwa,wote walistaajabu maana haikuwa kawaida kugongewa mlango usiku kama ule!
Wale mabinti walisimama wakamuangalia baba yao,mzee Jomo baada ya kuona macho yote yapo kwake akasimama kwenda kufungua mlango huku analalamika!
“Unaona sasa saivi mnanitolea macho mimi,angekuwepo kijana wa kiume hapa mngeniangalia hivi kweli!”
“Kwa mtoto wa kiume labda subiri wajukuu nadhani hata wewe unaona limeshindikana hili!”,alidakia mke wa mzee Jomo!
“Nani?”,aliuliza Mzee Jomo!
“Nifungulie nahitaji msaada!”
“Wewe ni nani?tatzo sizo kufungua tatizo namfungulia nani?”
“Mi…mi…ni mgeni hapa!”
Mzee Jomo aligeuka akaiangalia familia yake,wote walijiuliza ni mgeni gani wa usiku kama ule!
“Zubeda ebhu niletee panga langu chini ya uvungu!”
Alimuagiza binti yake mkubwa ambaye aliingia chumbani punde akarudi na panga na kumkabidhi baba yake!
Mzee Jomo alifungua mlango huku kashika panga lake mkononi,alikutana na sura ya kijana ambaye alikuwa mgeni kabisa machoni mwake!
Alipomuangalia hakumuona na kitu chochote chenye kudhuru,hakuwa na begi wala kitu chochote!
Alimuonea huruma kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha,akaamua kumkaribisha ndani,aliingia ndani wakampa kiti akakaa!
“Karibu kijana!”
“A…a…asa…nte!”
Aliitikia yule kijana huku anatetemeka kutokana na kunyeshewa na mvua ile kubwa kwa muda mrefu!
Wote walimshangaa alikuwa mgeni kabisa kwao,kijiji kile si kikubwa sana kwahiyo kama ni mgeni unajulikana haraka!
“Wewe ni mgeni hapa?”
“Ndi…o!”
“Umetokea wapi?”
“Ni…ni…mepotea!”
Yule mgeni aliongea kwa tabu kutokana na kupigwa na baridi la muda mrefu,Mzee Jomo alielewa hawataweza kuelewana katika mazingira kama yale!
Aliwaagiza wampe chakula wakampa wali na maharage uliokuwa umebaki,yule mgeni akala kwa pupa nkama mtu ambaye hajala muda mrefu sana,inaonekana alikuwa na njaa kali sana,alipomaliza alishukuru kisha Mzee Jomo akamchukua na kutoka naye nje muda huo tayari mvua ilikuwa imepungua!
UNAHISI MZEE JOMO ANAMPELEKA WAPI MGENI YULE WA AJABU?