Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI!
Sehemu ya 8
Mzee Jomo alitaka maelezo yaliyoshiba sababu kumpokea mtu kijijini bila kumfikisha kwa mjumbe au mwenyekiti ni kosa kubwa,mfano angefanya ubaya wowote ni wazi angewajibika yeye.Ndiyo maana alitaka maelezo ya kutosha kabisa ili ajiridhishe kuwa yupo na mtu salama!
“kijana jieleze vizuri bwana!”
Lukas alikohoa kidogo kurekesha koo kisha akajipanga kunyoosha maelezo ambayo hayakuwa na ukweli ndani yake,alichotaka ni kupata hifadhi ya muda mrefu ili aliyoyafanya mjini yasahaulike!
“Mzee wangu kama nilivyokwambia natafutwa na majambazi wanaotaka kuniua kisa mali za baba yangu,juzi nilivamiwa ndani kwangu bahati nzuri nikafanikiwa kutoroka,na kama unavyoniona sikubeba chochotye hata simu yangu niliiacha ndani,nilikimbia na nguo zangu tu nilizokuwa nimevaa!”
“Kwanini hukwenda polisi kutoa taarifa?”
“Mpaka sasa kifo cha wazazi wangu hakuna kilichotokea kabisa,tunazungushwa tu dana dana za kila siku na wauaji wanajulikana,ndiyo maana nilipovamiwa tu nikajua maisha yangu yako hatarini,nilikimbia mwisho nikaenda stendi nikapanda basi ambalo hata sikujua linaenda wapi?sikuwa hata na nauli nikashushwa porini na kujikuta nimefika kwenye hiki kijiji,naomba nafasi baba ninusuru roho yangu wataniua,walau nipotee kwa muda wanisahau!”
Aliongea Lukas kwa hisia na kumfanya Mzee Jomo amuamini aliyamwaga machozi kama mtoto,Lukas alilia kama mtoto!
Mzee Jomo alimuangalia bado hakuonyesha kama amekubali au lah!bila kusema neno aliinuka akaingia ndani na kumuacha Lukas akiwa na maswali mengi,hakuelewa kama amekubalika au lah!
Alichofanya ni kuendelea kuyavuta machozi kwa nguvu na kulia kwa hisia kali yote ni kuonyesha huruma ili ahurumiwe!
Mzee Jomo aliingia ndani aliporudi alitoka akiwa na familia yake yote,yeye mke wake na bintize wanne!
Alipofika aliketi kitako akakohoa kidogo kisha akamuangalia Lukas ambaye alikuwa kama mfungwa anayesubiri hukumu ya mwisho!
“Lukas!”
“Naa..m!”
“Naitwa Mzee Jomo huyu ni mkewangu na hawa ni binti zangu,historia yako imenigusa na nimeamua kukufanya mmoja kati ya familia yangu,utaishi hapa mpaka pale utakapohisi hali imekuwa shwari utaondoka!”
“Ahsante baba sijui nikushukuru vipi?”
Alisema Lukas akionyesha kufurahia kiasi akataka kupiga magoti kabisa kushukuru kupokelewa katika familia ile!
“Usijali kijana huna haja ya kunishukuru hivyo cha msingi ni kuzingatia heshima kuniheshimu na kuwaheshimu dada zako basi,pia usisahau hii ni SUMBAWANGA!”
Baada ya utambulisho ule Lukas aliingia kwenye kile kijumba alichopewa kuishi,alifika akaanza kurukaruka,alifurahi sana kuruhusiwa kukaa pale!
“Ooh!afadhali nijifiche kwanza huku maana moto niliowasha mjini hauzimiki leo,ila nitulie sasa Lukas dah,funga zipu Lukas!’”
Alijisemea Lukas kisha akajitupa kwenye kigodoro cha pamba akalala chali akaanza kuwaza namna alivyonusurika!
“Wanafunzi watatu wote wana mimba,kwa hiyo kila mwanafunzi miaka thelathini kwahiyo jela miaka tisini,bado yule mke wa mjeda ana mimba yangu yule mjeda anagenifuata jela aniambarruti bila mafuta yule,na yule mke wa jirani daaaah Lukas funga zipu sasa,ila ntaweza kweli maana mzee ana pisi kali tupu mmh Lukas tamaa itaniponza!”
*********
“Hivi mume wangu unamkubaliaje kirahisi ivyo je kama anadanganya?”
“Hapana machozi hayadanganyi mkewangu yule kijana ana shida ila kama anadanganya shauri yake hii ni Sumbawanga,itamfundisha kusema ukweli!
Mke wa Mzee Jomo alionyesha wasiwasi juu ya Lukas lakini mzee Jomo alimtetea,machozi ya Lukas yalimfanya amuamini moja kwa moja kabisa!
*********
Binti mkubwa wa Mzee Jomo alikuwa chumbani amejilaza,tayari taswira ya Lukas ilishamuingia akilini,alikiri ameona vijana wazuri lakini hajawahi kumuona kijana mzuri kama yule,alijikuta anamuwaza Lukas kwa hisia ambazo hakujua zim,etoka wapi!
Lukas alikuwa kijana mwenye sura iliyovutia hata umbo lake na urefu viliwachanganya sana wanawake,Lukas kilichokuwa kinamoponza ni kutokuwa mchoyo!
Alikuwa anampa kila mwanamke anayeonekana kulitaka penzi lake,hicho ndicho kitu kinachomponza siku zote!
Zubeda alionyesha kumpenda tayari kijana yule ambaye ndiyo kwanza ana siku ya kwanza pale kijijini!
“Mhh!ana kifua kizuri,mmh kale kasura kake jamani mmh!tutaonana wabaya tu kwa kweli hakuna jinsi!”
********
Mzee Jomo aliwaita binti zake akawaonya na kuwaambia wamuheshimu mgeni yule kama kaka yao,huku akiwasisitizia kuwa walikuwa wanataka kaka basi wamuheshimu Lukas kama kaka yao!
Kwa Zubeda ni kama hakuwa akisikia nini baba yake anasema,moyoni alishampenda yule kijana na alishaamua kufanya kila kitu ili mradi tu awe naye kimapenzi!
Mchana ulifika baada ya kuivisha chakula zubeda akatumwa kwenda kumuita Lukas aje kula,alifuirahi sana akatoka na kuelekea kwenye kijumba cha mgeni!
Alipofika hakugonga mlango,alipita moja kwa moja mpaka ndani na vile kile kijumba hakikuwa na sebule,moja kwa moja akajikuta yupo chumbani!
Hakuamini alimkuta mgeni akiwa mtupu kabisa hajajifunika chochote,alitumbua macho baada ya kuiona bakora ya mgeni ikiwa imening’inia!
Lukas alishtuka akajifunika shuka lakini tayari akawa ameshachelewa,Zubeda alishayaona maungo yake ya ndani na kubaki ameduwaa!
JE NINI KITAENDELEA?ITAKUWAJE KWA MGENI NA ZUBEDA!!