Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
Upo bi dada?...Huyu Kimox hapana wanawake tunawaonea sana yeye ni muhuniii af anamuacha mwnzie, Usjali ee Rozi mwaya angekuletea maradhi huyu nawewe uache bas hayo mawili matatu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upo bi dada?...Huyu Kimox hapana wanawake tunawaonea sana yeye ni muhuniii af anamuacha mwnzie, Usjali ee Rozi mwaya angekuletea maradhi huyu nawewe uache bas hayo mawili matatu
nipo askofuUpo bi dada?...
😎Umeshanogewa na ufirauni
Anatafuna exost tu [emoji23][emoji23]Umeshanogewa na ufirauni
tuko pamoja mkuu shukraniCHOMBEZO:
PAULA MFARANSA MWENYE VISA
SEHEMU 19
Mtunzi: Eng. Kimox Kimokole - 0786507507
Nikakanyaga mafuta mpaka Kivukoni nikaitumbukiza gari kwenye kivuko. Muda wote nawaza mahaba ya Habiba na namna alivyotaka kudanjwa kwa kitombo cha Mzaramo. Nikawa nawaza h lile tukio yaani kama picha ya Kihind hivi lakini ni kweli. Nafika home na kujibwaga kwenye sofa bado nikiwaza Kwampalange kwa Habiba namna kulivyosababisha tafrani kichwani mwangu.
Simu yangu inaita na kuitazama ni namba ya Rose nikaipotezea. Mara inaita namba nyingine nayo naipotezea, namba hii ndo iliita mara nyingi zaidi mpaka ikawa kero nikaona niipokee tu. “Haloo habari Kimox?” Ilikuwa ni sauti nzito ya kiume kutoka upande wa pili. “Salama, nani mwenzangu?” nikaisikilizia sauti ile ikiwa inashusha pumzi, “Mimi ni kaka yake Rose hapa, niko hospitali hali ya Rose ni mbaya sana. Hawezi kula na amedhoofu mno, amekuwa kwa siku hizi tatu anaishi kwa dripu tu.” Nikashusha pumzi na kumuuliza, “Upo hospitali umesema right? Kama upo wodini mpe simu Rose niongee naye...” Jamaa akampa simu Rose na kumwambia, “Kimox on the phone Rose, talk to him...”
Rose akaniita kwa sauti ndogo sana, “Kimox, samahani kwa yote, tafadhali naomba nisamehe. Sikustahili kukutendea vile, najuta kwa ujinga niliokufanyia. Sikulaumu kwa hatua uliyofikia ila nalaumu ujinga wangu mimi Rose...” Akapumua kidogo na kuendelea, “Nimekuwa mwanamke nisiye na heshima kwako, nimekutendea uovu sana ambao mwanamke hapaswi kumtendea mume wake ampendae. Nayajua maumivu unayoyapitia sasa hivi na hiko ndicho kinachoniumiza zaidi. Penzi langu kwako halikuwa la mzaha bali ni tamaa na vishawishi vya dunia vilivyonipofusha fikra zangu...” Rose akatulia kidogo. Nilinyamaza kimya namsikiliza bila kumkatisha chochote katika anayoyasema.
“Kimox, baada ya wewe kujua kile nilichokuwa nakifanya na uamuzi uliouchukua juu yangu nimegundua kwamba nimepoteza tunu muhimu sana. Nimepoteza mwanaume wa maisha yangu, nimepoteza mwanaume aliyenijali sana na kutaka kuniheshimisha, Nayakumbuka maneno yako yote sasa hivi uliyokuwa unayazungumza tukiwa pamoja na sasa yanajirudia kama mwamgwi kwenye ubongo wangu na masikio yangu. Kimox mimi Rose najihisi kama mjinga mbele ya dunia hii” akatulia tena. “Najua wanaume wako wengi na naweza kupata yoyote lakini si wa mfano wako, wewe ni wa kipekee na inaniuma sana kukupoteza... Kimox upo?” Nikamjibu, “Nipo nakusikiliza Rose vizuri sana...”
“Kimox, sikwambii samahani ili unisamehe na kunirudisha kuwa mpenzi wako la hasha, ninakuomba samahani kwa ujinga nilioufanya. Sikujua kwa hakika ni nini nakifanya na huenda ni sehemu ya funzo langu la maisha ambalo limenifunza katika njia ya kuumiza sana.” Akameza mate ambayo nilisikia namna alivyoyapitisha kooni kwa mshusho wa pumzi. “Mama yangu alijitahidi kukupigia ili angalau niongee na wewe. Naamini kuongea na wewe na kukuomba msamaha itakuwa ni tiba kwangu zaidi na huenda ikanipa nafuu. Siwezi kuyahimili maumivu haya moyoni mwangu na naamini yapo pia moyoni mwako kwa namna ile ile inavyoniumiza mimi... Kimox, nakujua una moyo mgumu sana na ni mwanaume unayeweza kuyahimili matatizo na misukosuko ya kila aina, una busara na hekima na maamuzi yasiyotetereka. Kwako najua hili litapita vizuri kuliko mimi lakini kwa siku ya leo nahitaji kuisikia sauti yako ikikubali msamaha wangu ili hata nikifa nife kwa amani ama kama nikipona basi niishi nikijua umeridhia msamaha wangu...” akapumua tena.
“Wewe ni mwanaume wa maisha yangu, sasa hivi ndo nahisi hilo ambalo mwanzo sikulihisi kabisa. Nimehisi penzi zito sana juu yako ambalo mwanzo sikuwahi kulihisi ingawa nimekuwa nawe kwa muda mrefu sana. Naomba ufahamu hili Kimox. Sikwambii sababu kwamba labda nahitaji kurejesha penzi hapana, nakwambia ili kuuweka ukweli huu wazi juu yako. Nilikuwa mjinga na kipofu, sikuona chochote lakini siku hizi chache nimegundua ujinga wangu. Kimox, kwa sasa nahisi kuutua mzigo ulionielemea moyoni mwangu na nayasema haya yote nikiwa na mama, baba, kaka na mdogo wangu wote wakisikia. Sihitaji kuficha katika kile nilichofanya juu yako, wazazi wanajua ujinga niliofanya na furaha niliyoipoteza.”
Mpaka hapo ndo nikajua kumbe aliongea haya wote wakiwa wamemzunguuka kitandani. “Kimox, asante kwa maisha yote uliyonipa na asante kwa penzi la dhati ulilonionesha katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Nitakukumbuka siku zote za maisha yangu kama bado nitaendelea kuwa hai. Nimewaambia wazazi na ndugu zangu wema wako juu yangu. Nimeweka wazi sababu nahitaji amani ya moyo. Nakushukuru sana!!!! NISAMEHE!!!!” Rose akamaliza kuzungumza na kuiacha simu bado ikiwa hewani kama anasubiri kusikia nitasema nini. Naamini muda huu aliweka simu kwenye sauti kubwa (Loud speaker).
“Rose, sina haja ya kusema namna ya penzi langu lilivyokuwa juu yako maana umesema yote na kwa hakika ndivyo ilivyo. Nimeyapokea maneno yako na yamejikita ndani yangu kwa utuo kabisa. Nimekusikia na kukuelewa kwa hakika ni nini umekisema. Nimepokea msamaha wako na nimeridhia, nimekusamehe kabisa kabisa kutoka ndani ya moyo wangu. Hakuna mwanadamu mkamilifu chini ya jua na hata mimi si mkamilifu kwa maana yapo mengi mabaya niliyoyafanya kama mwanaume na huenda tu wewe hukuwa na nafasi ya kuyaona ama kuyadhihiri kama nilivyofanya mimi” Nikatulia kidogo maneno yamuingie.
“Penzi letu limeingia doa kubwa sana hasa kwa mwanamke kuyatenda yale uliyoyatenda na haitakaa iwe sawa ama irudi kama zamani. Wanaume tunaumizwa zaidi tukisalitiwa katika namna ileilivyotokea ila kila mwanadamu anahitaji msamaha nami nimekusamehe Rose. Uwe na amani siku zote. Jambo la muhimu ambalo nahitaji ujue ni kuwa; Siwezi kukwambia kuwa nitakuwa nawe tena katika mapenzi, nina kinyaa mno na si rahisi tena kuwa na amani kama nilivyokuwa nayo awali na kwa hilo msamaha huu hauna maana nyingine zaidi ya kusameheana kama wanadamu ila si kurudisha mapenzi ya mke na mume. Things could not be the same again even if I intend to bring you back in my heart Rose.” Nikatulia kidogo na kusikilizia upande wake wa pili.
“Honestly, I love you... but I can’t hold it...” Rose akanikatisha, “I know Kimox, I know it and don’t say anymore...it’s OK!!! Lets take it as a lesson and start a new life. Thanks for everything Kimox.” Rose akatulia kwa muda kisha akakata simu. Nikatulia nikiiangalia simu kama naangalia mzimu wa Kolelo ya Bagamoyo au mizimu na vihenge vya Chief Maleare. Nikashusha pumzi nzito taratibu kabisa utadhani nilikuwa nammzigoooo na sasa nimeutua.
Nikampigia simu Paula tukaongea mengi akinihadithia mambo ya research yao na changamoto wanazokutana nazo kutoka Uziguani. Akanidokeza namna mbunge asivyo na ushirikiano na watu wake na kuwaunganisha watu katika kujiletea maendeleo. Paula ana upeo mkubwa sana wa kuchanganua mambo. Alitiririka point tupu na kuonesha njia mbadala katika kuinua maisha ya wananchi na hali zao. Akianisha tatizo la uongozi bora kama moja ya chanzo cha hali duni ya wakazi wale.
Kisha nikampigia Rahma na kumjulia hali akaniuliza kama Habiba alifika salama na hali yake. Nikamwambia nilimfikisha salama na sasa niko kwangu nataka nikapumzike kuweka mwili sawa. Tukaongea kwa bashasha halafu nikamuaga. Rahma akanipeperushia busu la huba nami nikalirejesha kwake akimalizia na neno zuri, “Kimox, nakupenda mpenzi wangu. Chochote katika maisha yangu nakifanya kwa ajili yako, wewe ndiye unayenipa sababu ya kuishi na kuyawazia ya kesho...Nakupenda mpenzi...!!” akaniambia kwa sauti ndogo sana na kunipa busu tena. Tukaagana na nikajongea kwenye chakula na mdogo wangu Kalunga kushibisha tumbo.
Asubuhi nimechelewa kuamka leo, sikujua kama muda umeenda kiasi hiki. Nikakurupuka na haraka haraka nikaanza kujiandaa kwa ajili ya kuwahi kazini. Ilishaimu saa mbili na dakika kadhaa na namna mshale wa saa unavyosogea sikutaka hata kuangalia mshale wa dakika unasemaje. Nilihangaika na uharaka wa kujiandaa kutoka tu basi. Kwa speed nikachomoka na kuwahi Kivukoni lakini nikakereka zaidi kukuta vivuko viwili viko upande wa pili na hiki kilichopo upande huu kimeshajaa na itanibidi kusubiri vile viwili vije huku vipakue abiria na magari halafu ndo sisi tuingie. Kibaya zaidi kuna meli kubwa ya mafuta inakaribia ili ikatie nanga bandarini hivyo lazima tusubiri hadi ipite ndo utaratibu wa kawaida uendelee. Sasa huo mwendo wa hili meli sasa ndo kero, kama konokono yaani.
Nikawasha redio kusikiliza vipindi vya magazeti redioni na kusikiliza taratibu za mazishi ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki juzi na Balozi Kijazi. Hivi vifo vimetutikisa sana sana yaani hata hatuelewi ni nini kinaendelea. Nikakumbuka barakoa yangu na kuiweka juu ya dashboard ya gari ili nikishuka ndani ya gari nivae tu. Nahisi hali ishaharibika na vifo vya hawa viongozi vilinipa hadhari huenda mambo si mambo. Natamani kila mmoja achukue tahadhari lakini nikitupa macho nje watu kila mtu na hamsini zake kama hakuna kitu vile.
Nikaingia ofisini nikipita walipo akina Nino na kuzikwea ngazi kuingia ofisini kwangu kwa majukumu ya kawaida. Baadae nikapiga simu kwa kina Nino kujua maendeleo ya Habiba na kumuuliza Nino kama ameshakunywa chai kwa kuwa mi sijanywa sababu ya kuwahi kazini. Nikaambiwa anaendelea vizuri tu na kuwa anashukuru kwa kumpeleka kwake jana, kwamba mimi ni mtu mwema sana. Nimechoma mafuta yangu kumpeleka Habiba bila gharama ni jambo la kipekee mno. Nikashukuru na mambo mengine yakaendelea.
Mchana nikampitia Nino na kumpeleka lunch halafu tukarudi. Mtoto ana raha sana sana na muda mwingi anatabasamu tu akiwa na mimi. Nikiwa ofisini kwangu Nino akanifuata na kuniinamia akanambia, “Jumamosi na Jumapili napenda kuwa na wewe, utakuwa tayari?” akanitazama na kuachia tabasamu. ‘Unamaanisha niwe nawe kwa usiku na mchana ama unamaanishaje?” Nikamtupia tena swali. “Ndiyo, niwe wako kwa siku hivo Jumatatu tunakuja wote kazini mpenzi...” Nino akasema akimwemwesa midomo. Nikamtazama kama siamini anachonambia huyu mwanamke. “Sawa mpenzi, haina shida. Ijumaa tutaweka mishe zote sawa kwa ajili ya hii appointment unayoniambia” akageuka na kuanza kuondoka. Mbele kidogo kabla hajakata kona akanitazama na kunikonyeza akitabasamu na kwa mwendo wa kimiss akapotea kwenye kona.
Nikabaki nawaza hiyo Jumamosi na Jumapili itakuwaje na tutakuwa wapi hasa. Je, nimpeleke home au lodge? Fikra zikawa zinagongana nikitafuta jawabu halisi. Mwisho nikaona mbona shwari tu kama itakuwa home maana Rose nishapiga chini na Paula hawezi kutokea sasa hivi kwa siku hizi akiwa kwenye kazi zake Tanga huko. Uamuzi ukaja ni bora nimpeleke kwangu tu ambako nitakuwa huru zaidi kuliko hotelini.
Itaendelea
Nishashusha cha weekend. Enjoytupia basi japo kimoja tena
shukran ila kila mwisho unakuwa mtamu sanaaa!hapo kwenye fumanizi nimejikuta na hasira kama mimi ndo nimefumania hizo chatiNishashusha cha weekend. Enjoy
Mimi nimejiona kama ndo nimefumaniwa vile...shukran ila kila mwisho unakuwa mtamu sanaaa!hapo kwenye fumanizi nimejikuta na hasira kama mimi ndo nimefumania hizo chati
Hatari sana yaani. Usiombe yakutokee bhanashukran ila kila mwisho unakuwa mtamu sanaaa!hapo kwenye fumanizi nimejikuta na hasira kama mimi ndo nimefumania hizo chati
Aiseee, pole sanaMimi nimejiona kama ndo nimefumaniwa vile...