Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Cha kwanza wameenda ,hayo mengine ubongo utazidi kuchapa kazi,hata robots wanaweza kuwekwa huko au anything different
Majuzi niliona bbc wanataka waanze kuunganisha genes za binadamu na wanyama wengine Ili kitokee kiumbe mpya
Hapa tuu duniani watu wanazaliwa bila kukutana kimwili mbegu zinaunganuishwa anatokea binadamu sasa hilo la kwenda kuwazalisha huko huoni ni rahisi zaidi?
Utafikaje kwani huoni zamani wakati wanaanza utafiti it used to take years kufika Mars sasa hivi ni miezi ko tech unakua na itaboreshwa zaidi.
Rocket za vita zinatumia chini ya saa moja ku hit target ya bara moja Hadi jingine ndio watashindwa vipi ku improve speed hapo?
Eti sayari 9,utafiti umeonesha ziko 11 hizo tisa wewe umezijuaje bila wazungu kukuambia? Utafiti unaonesha huenda kuna zaidi ko kadiri Sayansi inavyokua mambo mengi yatazidi kufahamika
Nasema tu hivi kuwa hii sayansi ni kubwa tena kubwa sana kwako pia acha mambo ya imani na sayansi. Level zako za kufikiria inaweza ikawa chini. Huwezi ukafikiri vitu vikubwa wakati vidogo huvijui.Naanzia hapa,suala la budget waesema lini au umejiaje kama budget ni kubwa ? Umbali wa kwenda Mars na Mwezini unatofautiana vipi na changamoto ni zipi ? Bajeti hiyo ni kiasi gani wanayo
Kuna swali nilikuuliza wewe unahihikisha vipi ya kuwa kweli wameenda Mwezini au Mars ? Marejeo yako wewe ni yapi ? Hili swali hujalijibu. Kwamba je kwa kuona picha au kusikia habari ?
Hapa naona unawachoresha Wanasayansi na kuwafanya tuwaone wamebweteka. Kisayansi walitakiwa mpaka sasa hivi wawe wameshaenda zaidi ya mara kumi sababu ni zaidi ya miongo mitatu tangu tuambiwe Nail alikwenda mwezini. Maana yake walitakiwa wawe wameshabuni vifaa vyenyw ufanisi mkubwa na kwa gharama nafuu. Labda watuambie ya kuwa gharama imekuwa kubwa zaidi ya kuandaa movie kama hiyo, au wameshajua ya kuwa watu wameshawaona wao mazwazwa kwa kuigiza tukio hilo pale Area 51.
Lakini suala la uzandiki juu ya tukio la mwezini mbona limeshabatilishwa tangu zamani na husemwa pia sababu ya kifo cha John F. Kenedy ni kufichua siri au kutaka kufichua mbinu hiyo. Kihistoria husemwa ya kuwa hiyo ilikuwa ni vita baina ya USSR na Marekani katika kuonyeshana umwamba maendeleo ya kisayansi.
Mimi siyo kwamba nadhani bali nina uhakika kabisa.
Watuambie kwanza umbali wa kutoka katika uso wa dunia mpaka mwezini ni kiasi gani ? Bila kuweka Assumtions yoyote ile, wakiweka tu Assumptions wameharibu.
Pili, walitumia vigezo gani kutengeneza kifaa ambacho walijua fika kitawapeleka na kuwafikisha mwezini ? Hapa inabidi watuambie. Maana yake kabla inabidi ufanya ufanue utafiti, na utembelee sehemu husika. Tafiti hii ilifanyika wapi na kwa kutumia nini ?
Sasa unapohoji haya mambo ndipo unapoona ya kuwa hili ni igizo na wengine walithibitisha hilo.
Tatu, kiimani jambo hili hali wezekani, sababu hakuna anaejua ya kuwa Mwezi uko umbali gani toka mbingu ya kwanza ila kwa macho ukiangalia vizuri unaona ya kuwa mwezi uko karibu sana na mbingu ya kwanza kuliko ardhini, yaani duniani. Tunaambiwa umbali wa mbingu ya kwanza na dunia na mbingu na mbingu ni mwendo wa miaka 500. Hii ni kwa mwendo kasi wa juu zaidi (Rejea jaya katika kitabu kiitwacho "Qamus al Bida'ah" ). Maana chini ya muda huo hizo zinabaki kuwa stori tu na kufurahisha nafsi.
Tatu, zipo sababu za kisayansi zinazo pinga igizo hilo. Unaweza kuzifatilia Google ukazipata. Ukisearch "Did we land on the moon". Utaona mambo mengi wapo wanao thibitisha ya kuwa tukio hilo ni kweli na wale wanao kadhibisha tukio hilo, ukipima katika mzani utaona ya luwa hawa wapili wana hoja zenye nguvu mno kuliko wengin, na hao wa kwanza wameanza kuja kuandika hayo hivi karibuni.
Narudi kuendelea hapa nilipoishia...
Ndugu naona unajisumbua na huyu mtu, nimesoma comments zake nikajua anacho kiandika pia hakijui, yaani eti ikipita mawingu ndo mbinguni. Nahisi hajawahi hata kupanda ndege, maana angekuwa anewahi kupanda ndege angekuja na kusema amefika mbinguni maana aliyaona mawingu yakiwa chini na yeye alikuwa ameyavuka mawingu. Inasikitisha sana ukipita mawingu utakuwa umefika mbinguni!!!!!!!!Kwa hiyo wewe akili zako Mbinguni ukishapita mawingu umefikaa???[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
We darasa la saba hata haujamaliza, kwanza haujui hata sayari ni niniWewe nae unaamini huo uongo [emoji23][emoji23]
Umeleza vizuri ila sisi tulio soma historia za mangungo wa msovero tutakuona unaongelea story tu, kumbe kuna complex calculation mpaka kufikia hivyoUkimfuatilia elon musk utaona anahangaika kuland ile prototype yake ya Spaceship inaitwa Starship ni bonge ya kipande cha chuma chenye 122m.
Zile starship ndio atatumia kupeleka watu mars kwenda kufanya uchunguzi, planetary engineering, kutengeneza mji pia kufanya repopulation.
Right now bado anafanya landing test na belly flop manoeuvre kwa ajili ya mars atmospheric entry.
SN 8 imefail kuland na SN9 imefail lakini bado anaendelea kufanya test hivyo SN10 soon italaunch.
YouTube wanaoneshaga live kutoka boca chica.
Na haiwezekani kutumia ndege sababu ndege na engine zake haziwezi kufanya kazi au kupaa bila air resistance.
Na nje ya earth's atmosphere hakuna air resistance ni vacuum.
Hivyo ndio sababu wanatumia rockets.
Pia sio wote ambao wataenda huko mars hata kama ikitokea catastrophic event hapa duniani.
Lakini Itategemea na technology ya kipindi hicho na ukubwa wa hivyo vyombo.
We darasa la saba hata haujamaliza, kwanza haujui hata sayari ni nini
Huwa nawaona wajinga kwa sababu nyingi sana. Hizi ni miongoni mwazo.Nasema tu hivi kuwa hii sayansi ni kubwa tena kubwa sana kwako pia acha mambo ya imani na sayansi. Level zako za kufikiria inaweza ikawa chini. Huwezi ukafikiri vitu vikubwa wakati vidogo huvijui.
Tuanze na vitu vidogo vidogo kama kwanini gari linatembea kwa kutumia mafuta na mafuta yanafanyaje mpaka litembee.
nguo zako zinatengenezwaje mpaka ukapata cha kuvaa badala ya kutumia magome ya miti.
Bila shaka unaweza ukabisha kuwa hakuna Marekani kwa kuwa wewe hujafika huko Marekani?
Hebu jiulize ndege inafanyaje mpaka ikapaa na unatumia muda mchache tu kutoka bara moja kwenda jingine?
Ukipata majibu yitu vidogo ambavyo unaweza ukaviona nahisi utaelewa hata mambo makubwa, pia naona ulikimbia sayansi toka shule ya msingi Ndio maana hata sayansi yetu ya nadhalia inakushinda sasa ya vitendo utaelewa kweli?
Nchi nyingi saivi zimepeleka vyombo vyao mwezini ikiwemo Russia na China, tena China chombo chake kimekuja na sample kabisa.
Mwisho sisi tuwaachie wakubwa wa sayansi wafanye yao na tubaki tunatazama tu huku hata uhakika wa kesho yetu hatujui.
Hizi sio akiliwewe umezihakiki vipi hizo habari za kwamba je ni kweli au umetosheka na kusikia au kuona tu ?
Naendelea kufurahu na kuwaona hamna mnachokijua, na unachokiandika ni dhana na laiti kama ungekuwa umesoma nilichokiandika usingeandika au kuhoji kitoto namna hii. Nakukumbusha tu japokuwa unadai ya kuwa umesoma nilichokiandika. Nimesema haya yafuatayo :Ndugu naona unajisumbua na huyu mtu, nimesoma comments zake nikajua anacho kiandika pia hakijui, yaani eti ikipita mawingu ndo mbinguni. Nahisi hajawahi hata kupanda ndege, maana angekuwa anewahi kupanda ndege angekuja na kusema amefika mbinguni maana aliyaona mawingu yakiwa chini na yeye alikuwa ameyavuka mawingu. Inasikitisha sana ukipita mawingu utakuwa umefika mbinguni!!!!!!!!
Hizi sio akili
Wewe ndio inatakiwa utoe ushahidi wako kuwa sio kweli.
Kabla sijakujibu swali lako kwanza nataka unieleweshe na kunipa sababu za kuwa una akili nyingi kuliko Einstein. Umetumia standard gani kupima mpaka kufikia hitimisho kuwa una akili nyingi kuliko Einstein?Huwa nawaona wajinga kwa sababu nyingi sana. Hizi ni miongoni mwazo.
1. Hamjui kuhoji na kutafuta ukweli juu ya habari mnazo zisikia, na hili wahusika wamefanikiwa sana, sababu wameona wengi wenu mnapenda kuona.
2. Hamjibu maswali ninayo wauliza zaisi ya ushabiki kwenye Sayansi.
3. Mnatakiwa kuvunja hoja na kuweka ukweli na si kinyume chake, kama mnavyofanya nyinyi. Mathalani nikikuuliza wewe unahakikisha vipi ukweli wa hizi habari ? Bila shaka kwenu nyinyi mnazipokea tu, hili ni tatizo lenu binafsi na ukameme wenu. Kuna mmoja niliwahi kumuuliza anadai ya kuwa Albart Einstein alikuwa na akili sana, nikamwambia nitajie mambo matano ambayo aliwahi kuyasema au kuyafanyia utafiti halafu yakawa kweli, kisha nikamwambia mimi binafsi Einstein hanifikii kwa akili, na hakuna atakaye weza kuthibitisha ys kuwa Einstein kanizi mimi akili.
4. Huwa mnatatizo au matatizo ya kulinganisha mambo hasa katika kutoa mifano. Mifabo yako yote ni mfu sababu unalinganisha uhalisia na na visivyo halisi, mangapi au vingapi hatujawahi kuvidiriki na tunaviamini ? Achilia mbali tu hapo Marekani. Mimi nina muamini Mtume na yote aliyokuja nayo lakini sijawahi kumuona, tunaamini uwepo wa kina Plato, Socrates, Anaksimenesi na wengine katika Wanafalsafa wa magharibi na wasio kuwa hao, lakini hatujawaona. Sasa mnapokosa hoja bora mnyamaze na mimi na nyinyi tunatofautiana pakubwa sana, mimi natafakari na kuhoji kwa usawa nyinyi ni mashabiki, na wakubwa zenu wanawapa kile mnachokitaka.
Mwisho kabisa nakuuliza swali dogo ambalo wenzako wamelikimbia, wewe umezihakiki vipi hizo habari za kwamba je ni kweli au umetosheka na kusikia au kuona tu ?
Kwa faida yako soma soma hata Kepler's laws of planetary motion, ndo hizo zinatufanya kujua umbali na kuweza ku peleka setilite huko juu na zikakaa tunapo taka zifike, bila assumptions kwenye science haiendi maana vitu havipo linearly kama unavyo taka ila sijui kama umenipata. ila kama haya mambo yamekupita kushoto, itakuwa ni kazi buleNaendelea kufurahu na kuwaona hamna mnachokijua, na unachokiandika ni dhana na laiti kama ungekuwa umesoma nilichokiandika usingeandika au kuhoji kitoto namna hii. Nakukumbusha tu japokuwa unadai ya kuwa umesoma nilichokiandika. Nimesema haya yafuatayo :
1. Ukiangalia kwa macho unaona ya kuwa Mwezi upo karibu sana na Mbingu kuliko dunia, nikahoji watuambie umbali halisi bila kuweka "Assumptions" zozote wa duniani mpaka mwezini.
2. Nikasema ya kuwa umbali mbingu moja kwenda mbingu nyingine na kutoka duniani kwenda mbingu ya kwanza kwa mwendo kasi wa juu zaidi ni miaka 500. Sasa kama una akili vizuri na kutafakari utaelewa nini nakusudia.
3. Kupanda ndege hakukufanyi ukajua mbingu iko mbali gani na Sayansi yenyewe haijui, ndiyo maana hata hao NASA wanaendelea kuleta maigizo. Kwahiyo hizi mada zinataka hoja na si viroja na kuimba mapambio.
4. Ninajua ninachokihoji, kama huamini tuendelee na mjadala.
Atakuwa ana comment akiwa ziarani marshii lugha sio ya nchi hii
Sababu ziko nyingi, hizi baadhi.Kabla sijakujibu swali lako kwanza nataka unieleweshe na kunipa sababu za kuwa una akili nyingi kuliko Einstein. Umetumia standard gani kupima mpaka kufikia hitimisho kuwa una akili nyingi kuliko Einstein?
Hapo ndo nitapata sehemu ya kuanzia kukupa maarifa ya logic reasoning, bila hivyo itakuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa
Kijana labda nikusaidie kitu kimoja ili usipoteze muda katika hakuna, usiniwekee mambo yenye "Assumptions" weka uhalisia wa mambo, haya mambo nimeishi nayo ila nilipoanza kutafakari kwa usahihi na kuhoji na kusoma vitabu vya wakubwa nikajua ya kuwa huo ni utoto.Kwa faida yako soma soma hata Kepler's laws of planetary motion, ndo hizo zinatufanya kujua umbali na kuweza ku peleka setilite huko juu na zikakaa tunapo taka zifike, bila assumptions kwenye science haiendi maana vitu havipo linearly kama unavyo taka ila sijui kama umenipata. ila kama haya mambo yamekupita kushoto, itakuwa ni kazi bule