Chomete atembelewa na madiwani wa halmashauri ya mji wa Tarime-Bungeni Dodoma

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
MHE. GHATI CHOMETE ATEMBELEWA NA MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME-BUNGENI DODOMA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe. Ghati Zephania Chomete ametembelewa na Wahe.Madiwani wakiongozwa na Mhe.Thobias Elias Ghaty- M/Kiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Madiwani hao walifika Bungeni kwa ajili ya kujifunza uendeshaji wa shughuli za kila siku Bungeni, Kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na Waziri wa Ujenzi kwa lengo la kuwasilisha changamoto zinazowakabili na ambazo zimekuwa kero ya muda mrefu katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Madiwani hao wamewasilisha changamoto hizo kwa Mhe. Dkt. Festo Dugange - Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na Mhe.Godfrey Kasekenya (Eng) - Naibu Waziri wa Ujenzi.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…