Jalema
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 594
- 868
Hapa nilipo ni mwezi sasa unakatika kila siku lazima nimeze diclopa mbili asubui na jioni laa sivyo nitashindwa hata kuamka kitandani maana maumivu ya kichwa yananisumbua kweli kweli napata mafua mazito sana yanayokaribia kukauka mda mwine yanakua kama na mchamchanga na vumbi na kila nikivuta pumzi naskia mishipa yote ya kichwa inauma huku kichwa kinagonga kisawasawa sina stress yoyote,sijaachwa na mwanamke wala sijasalitiwa wala sina jambo ninalowaza sana mpaka kufikia huko maana wengi wanasema ndio sababu labda nilisha kwenda hospitali kubwa nikapima kila kitu macho, damu,mkojo,kinyesi, yaan nilipima kila kitu wakaniambia hawaoni tatizo kuanzia kichwani mpaka mwili wote na wakaniambia hicho sio kipanda uso wakanipiga pain killer wakanipa vidonge vinaitwa ubprofin, nimemeza vyote lakini nafuu sijapata nimerudi kwenye diclopa msaada wataalam naomba maana naona nikiendeleza kumeza ivi vidonge kila siku vitakua sumu mwilini