Chonde chonde msibadili alama ya ufaulu kidato cha pili

Chonde chonde msibadili alama ya ufaulu kidato cha pili

mamayeyo

Senior Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
167
Reaction score
138
Kwa uchungu na masikitikomakubwa nasikia matokeo ya darasa la saba yalirekebishwa ili kufuta aibu kwani wengi walikuwa chini ya wastani unaotakiwa ambao ni 100/250. Habari za kuaminika toka wasahihishaji wa mitihani ya kidato cha pili ni kuwa wanafunzi wengi sana wamekosa wastani unaotakiwa kuingia kidato cha 3 mwakani ambao ni alama 30.
Nahofia kuwa wahusika watataka kuficha hii aibu kwa kuteremsha alama za ufaulu. Chonde chonde msifanye hivyo. Hao waliopata wastani wa 30 na kuendelea ndio watakaopambana na kitabu ili walau kupunguza division zero mwaka 2014. Na hao waliofeli na kurudia kidato watapambana zaidi na hatimaye pumba itachekechwa na mchele mzuri utabaki. Mimi nina hakika hao waliochakachua matokeo ya darasa la saba watachakachua na ya kidato cha pili pia. Nani anabisha?
 
Kwa kuwa hawa magamba wanatafuta kujikweza zaidi kisiasa tegemea uchakachuzi tu na kama sivyo si ajabu tukaambiwa kuwa ufaulu umeogezeka na wanafunzi wote wamefuzu kuingia kidato cha tatu. Magamba ni hatari kwa ustawi wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom