Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio utauvunja Muungano

Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio utauvunja Muungano

Mkuu kosa la jk liko wapi kazi iko mezani wajumbe wanaendelea na kazi wao wanajukumu la kupima na kuamua kilicho chema wala siyo vinginevyo hayo mawazo yako ya kurushia watu lawama bila sababu hazina maana.

Jk ni mwenyekiti wa ccm na kinachogomba bungeni ni kulazimisha rasmu ya ccm ya serikali 2 .
 
Pasco

Si tu utavunja muungano. Bali utasababisha machafuko endapo CCM watalazimisha sera zao dhidi ya maoni ya wananchi. Hali inaweza kuwa mbaya sana iwapo CCM wataendelea kuchezea mamlaka ya watu.

Naona TBC wamekata tena....naambiwa TBC Taifa walikata saa 9.15.
 
Pasco, kuna mwanaCCM, kw mdomo wake na kwa masikio yangu alini imanisha kuwa wameandaa both plan. Plan A serikali 2, hivyo kuimarisha muundo uliopo, na Plan B serikali 3 na tayari wameandaa jinsi ya kujipanga, ikiwemo kule zanzibar kuhakikisha CUF hawapati kura za kutosha, na hasa kutumia mafanikio ya SUK.

Pasco kwa bandiko lako, umejibu swali langu moja, ambalo ni kwanini CCM wameingia kwa kukebehi ile rasimu ya Katiba ya Jaji J.W? na kwanini wameingia bungeni na msimamo mmoja, kama kweli walikuwa na hizo plan?. Zaidi ya hapo mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, hawezi kufanya jipya tena kwa sasa. kama ni wahafidhina walimshauri basi ujue amekula sumu ya kutosha na ng'ombe wetu ndo kapandwa mwezi uliopita hivyo hatuna mziwa. hapo ni kusambaza taarifa ya msiba na kuomba kauli ya mwisho ya mgonjwa.

Ushauri wako umefika na ni mzuri lakini wakati siyo mwafaka kwa sababu;
1. msimamo huu umekuwa ni wa chama wamekubaliana kwenye kamati kuu na mpango ulitengenezwa ikiwemo kundi la 201, idadi ya wabunge na kuamini watashinda bungeni kwa wingi na si kwa hoja.
2. kuna wale wenye free mind (umemtaja Sita) ambao walitaka serikali 3, ila wakashindwa na maamuzi ya chama, kubadili kauli ya sasa ya CCM italeta ufa mkubwa sana ndani na nje ya chama, madhara yake makubwa na mengi ikiwemo baadhi ya wanachama kujitoa au kulaani au kujigamba hadharani na hiyo ni tafrani
3. Mh. Rais Jakaya Kikwete alihutubia taifa kupitia bunge la katiba, nchi nzima iliona na kusikia siyo maneno yake na msimamo wa chama chake tu, bali kebehi na maneno makali kwenye rasimu ya jaji, si hivyo tu Vigelegele, vifijo na miluzi vilitawala, je leo atatoa kauli gani kupindua hiyo hotuba?
4. Katibu wa CCM mh A. Kinana na katibu mwenezi Npe NNauye, wapo mikoani kuomba ridhaa ya wana CCM, kupigia kura rasimu yenye serikali 2, maana ndo maamuzi na mpango wa CCM. Je Pasco unataka katibu afanye nini tena?
5. Ushauri wako ukifuatwa, Mh Jakaya Kikwete asitoe kauli hiyo, (kwa sababu mazingirz aliyotengeneza kwenye uzinduzi wa BLK) Katibu wa CCM mh Kinana hawezi toa kauli hiyo, angalia namba 3. Nape najua kabisa hatadhubutu, na wewe unajua. Swali kwa chama nani atatoa kauli tofauti ya serikali 2?
6.kama m/kiti mh S. Sitta wa BLK atapitisha rasimu ya serikali tatu yeye na wajumbe wake mle ndani ya bunge wataonekana wasaliti, na wawakilishi watonekana kushindwa kazi, zaidi ya hapo CCM wataona kama UPINZANI nchini umeshinda, hivyo wemepoteza dola!!

Botom line hakuna mwenye kubadili mawazo ya CCM, hivyo tegemea kutokea kwa unabii wako, endapo uko sahihi!!
Its broken can't be fixed................. i know you all know what to do

Sp
 
Mkuu kosa la jk liko wapi kazi iko mezani wajumbe wanaendelea na kazi wao wanajukumu la kupima na kuamua kilicho chema wala siyo vinginevyo hayo mawazo yako ya kurushia watu lawama bila sababu hazina maana.
Rejea kwenye hotuba ya JK ya kuzindua bunge la katiba unaweza ukanielewa nazungumzia nini.
Pia rejea jinsi Ikulu ilivyo 'mshit' Jaji Warioba baada ya kuwasilisha kazi waliyompa.
 
Katiba ya Tanganyika itakuwa lahisi .unaondoa neno serikali ya shirikisho halafu vifungu vyote vinabaki kama vilivyo full stop.
 
Mkuu Pasco,

Katika kosa kubwa JK alifanya ni kuruhusu mchakato wa katiba uende kwa usawa bila CCM kuingilia au kutia hila! Nadhani walidhani itakuwa rahisi katika BMLK!! Well, naona kama tunavyoona inathibitisha kuwa ni hata ri tupu!!

Ushauri wako kwake ni kweli tupu, kweli chungu kuimeza, lakini ndo njia pakee. WaZNZ hapa ndo njia pkee wanayoiona, na sidhani kama watakubali this time!

Maamuzi ni yao...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco bandiko nalikubali kwa asilimia 100. Natamani mkuu angeliona na kuzingatia yote uliyoeleza, lakini kwa kuwa sikio la kufa halisikii dawa basi sitegemei lolote toka kwake. Hoja namba sita ni imani yangu siku zote.
 
Muungano lazima uende mkuu Pasco, kama muungano autoenda kuna wengi urais watausikia kwenye bomba, maana watapewa wengine kwa maudhui ya kulinda muungano, hii katiba kiukweli ccm hawakujinga, inawatwanga kotekote
 
Pasco, kuna mwanaCCM, kw mdomo wake na kwa masikio yangu alini imanisha kuwa wameandaa both plan. Plan A serikali 2, hivyo kuimarisha muundo uliopo, na Plan B serikali 3 na tayari wameandaa jinsi ya kujipanga, ikiwemo kule zanzibar kuhakikisha CUF hawapati kura za kutosha, na hasa kutumia mafanikio ya SUK.

Pasco kwa bandiko lako, umejibu swali langu moja, ambalo ni kwanini CCM wameingia kwa kukebehi ile rasimu ya Katiba ya Jaji J.W? na kwanini wameingia bungeni na msimamo mmoja, kama kweli walikuwa na hizo plan?. Zaidi ya hapo mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, hawezi kufanya jipya tena kwa sasa. kama ni wahafidhina walimshauri basi ujue amekula sumu ya kutosha na ng'ombe wetu ndo kapandwa mwezi uliopita hivyo hatuna mziwa. hapo ni kusambaza taarifa ya msiba na kuomba kauli ya mwisho ya mgonjwa.

Ushauri wako umefika na ni mzuri lakini wakati siyo mwafaka kwa sababu;
1. msimamo huu umekuwa ni wa chama wamekubaliana kwenye kamati kuu na mpango ulitengenezwa ikiwemo kundi la 201, idadi ya wabunge na kuamini watashinda bungeni kwa wingi na si kwa hoja.
2. kuna wale wenye free mind (umemtaja Sita) ambao walitaka serikali 3, ila wakashindwa na maamuzi ya chama, kubadili kauli ya sasa ya CCM italeta ufa mkubwa sana ndani na nje ya chama, madhara yake makubwa na mengi ikiwemo baadhi ya wanachama kujitoa au kulaani au kujigamba hadharani na hiyo ni tafrani
3. Mh. Rais Jakaya Kikwete alihutubia taifa kupitia bunge la katiba, nchi nzima iliona na kusikia siyo maneno yake na msimamo wa chama chake tu, bali kebehi na maneno makali kwenye rasimu ya jaji, si hivyo tu Vigelegele, vifijo na miluzi vilitawala, je leo atatoa kauli gani kupindua hiyo hotuba?
4. Katibu wa CCM mh A. Kinana na katibu mwenezi Npe NNauye, wapo mikoani kuomba ridhaa ya wana CCM, kupigia kura rasimu yenye serikali 2, maana ndo maamuzi na mpango wa CCM. Je Pasco unataka katibu afanye nini tena?
5. Ushauri wako ukifuatwa, Mh Jakaya Kikwete asitoe kauli hiyo, (kwa sababu mazingirz aliyotengeneza kwenye uzinduzi wa BLK) Katibu wa CCM mh Kinana hawezi toa kauli hiyo, angalia namba 3. Nape najua kabisa hatadhubutu, na wewe unajua. Swali kwa chama nani atatoa kauli tofauti ya serikali 2?
6.kama m/kiti mh S. Sitta wa BLK atapitisha rasimu ya serikali tatu yeye na wajumbe wake mle ndani ya bunge wataonekana wasaliti, na wawakilishi watonekana kushindwa kazi, zaidi ya hapo CCM wataona kama UPINZANI nchini umeshinda, hivyo wemepoteza dola!!

Botom line hakuna mwenye kubadili mawazo ya CCM, hivyo tegemea kutokea kwa unabii wako, endapo uko sahihi!!
Its broken can't be fixed................. i know you all know what to do

Sp
Swiper,

Mtazamo wangu ni kama ifuatavyo:

Katika nyakati hizi, ccm haina ujanja wa kutafuta any other source of legitimacy kutawala zaidi ya Katiba ya nchi kupitia dhana ya "constitutionalism". Waligundua hili mapema, hasa baada ya kubaini kwamba all othe sources of her legitimacy zimekwenda na maji, yani:
A) Integrity and charisma ya Mwalimu Nyerere. Chama kimeshidwa groom watu wa aina hii kwani hakiwahitaji tena, wataharibu mpango wao wa kuegemea matajiri, mafisadi na wawekezaji badala ya wakulima ma wafanyakazi.

B) source ya pili ilikuwa ujamaa/azimio la arusha, nayo chama kimeliua na kuleta azimio la zanzibar ambalo limehalalisha ufisadi na wizi wa mali ya umma.

C) source ya mwisho ya legitimacy ya ccm kutawala ilikuwa ni historia ya TANU na baadae CCM (hadi 1985) katika kutetea wanyonge ndani na nje ya nchi. Wanyonge hawana lao tena ccm leo hii.

Hizi zilikipa ccm uhalali wa kutawala, kuunda serikali, kuchakachua mambo n.k, bila ya kujalisha katiba ya nchi kwani wananchi waliamini zaidi katika nguzo zile kuu tatu. Ccm kujua hazipo tena na chadema kuzidi kupigania katiba mpya, wakaona wadandie treni hiyo hiyo wakijiamini kwamba wataielekeza Final destination iwe LUMUMBA. Treni ingeweza kwenda lakini abiria wameanza kushuka (rejea maoni ya wananchi ndani ya rasimu). Pamoja na hayo, ccm inaendelea kuamini (which I agree as well) kwamba hakuna source iliyobakia ya legitimacy nyakati hizi zaidi ya Katiba inayoungwa mkono na wananchi walio wengi. Mkakati wa ccm kuhakikisha mtazamo wake unaungwa na walio wengi umekwama. Kwanini? Huo ni mjadala mpya, lakini unachangiwa na kumomonyoka kwa zile three sources of legitimacy that the party had huko nyuma.

Nini kitafuatia? Yawezekana ukawa sahihi lakini kwa mtazamo wangu pengine finyu, kitendo cha ccm kukubali serikali tatu haitakipa chama tena moral authority kupanda jukwaani kugombea urais wa Tanganyika, labda wa muungano. Utaendesha kampeni gani kwa serikali uliyoikataa? Tanganyika itaenda kwa chadema, lakini hasa iwapo itashirikiana na CUF. Zanzibar itaenda CUF kwa sababu zile zile - CCM ni adui wa rafiki wa waznz walio wengi yani "serikali tatu" kwani wanajua kwamba bila ya serikali tatu, hakuna mamlaka kamili znz, itaendelea kuwa porojo tu.

Katika wana ccm, serikali tatu zikipitishwa, hawatokuwa na jinsi bali kumsimamisha sitta ambae hajachafuka sana na usaliti wa Tanganyika, au Membe ambae amekuwa mjanja kukimbia hoja ya serikali tatu ili asieleweke msimamo. Magufuli na Mwandosya wanafuatia kwa mbali.

Chini ya serikali tatu, lowassa, tibaijuka, nchimbi, makamba, wassira, mwakyembe, wote hawa wameshasaliti Tanganyika, wakipanda jukwaani kuombea kura urais wa Tanganyika watarushiwa mayai viza.

Lastly, CCM haiwezi zuia serikali tatu bungeni, wameshindwa. Kwa mtazamo wangu, kwa sasa mikakati ni to sensitive umma ili ikifika siku ya kura ya maoni, kura za serikali tatu zisitoshe, kihalali au kihilali.
Nguruvi3

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mode: Naomba nirekebishie headline ya bandiko hili isomeke

CHONDE CHONDE JK!, MSIMAMO WA CCM WA SERIKALI MBILI, NDIO UTAKAOVUNJA MUUNGANO!.

Pasco
 
Pasco sikuwa nimesoma uzi wako. uko sahihi kabisa. Wanachofanya wahafidhina wa CCM ni maandalizi ya kufutwa kwa chama hiki kikongwe huko Zanzibar. Hata kwa kura za maruhani CCM will not make it, 2015 chini ya serikali 2. Tutawakumbusha!
 
Last edited by a moderator:
Bjpi5YNCEAA2kY6.jpg

hiii ni nini sasa!!!!
 
Back
Top Bottom