Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio utauvunja Muungano

Ok, hiyo ya Zanzibar ilitoka mbingunu? si waliandika nasi tutaandika

Sawa

Lakin pamoja na yote

Tukikubaliana kuwa na serikali tatu tukumbuke kwamba hatuna katiba ya Tanganyika

Wezentu wazanzibar wanayo katiba yao,ukiachilia mbali katiba hii bado tunayo kazi nyingine na kuiunda katiba ya tanganyika pia
 
Ok, hiyo ya Zanzibar ilitoka mbingunu? si waliandika nasi tutaandika

lin sasa mutaandika??

maana sasa tunaandika katiba ya jamhuri ya muungano,zanzibar wanayo tayar

tukipata ya jamhuri ya muuungano kwa kigezo cha serikali tatu ya tanganyika itapatikana lini na tanganyika itajiendeshaje bila katiba.
 
Pasco your are the bomb!!!!,mimi binafsi nilikuwa nna mawazo kama yako kuhusu CCM na matakwa yao ya kutaka mungano ubakie kama ulivyo

Kiukweli kama CCM haitaikubali rasimu ya Warioba ndio mwisho wake kisiasa,wazo langu bora CCM ife ikiwa inakumbukwa na watanzania kuliko kufa kifo cha kusahaulika kabisa kisiasa..... wenzetu wamesema "If you can't beat them join them"

Mungu ibariki Tanzania
 
Wakati Zoezi la kupiga kura likiendelea, najikumbusha kidogo baadhi ya hoja za msingi kuhusu katiba!.

Pasco
 
Mkuu Kobe, posti yako hii, nimeikuta mahali, nimefurahishwa sana na hoja yako ya msingi, haswa pale ulipozungumzia, uelewa mdogo umaskini, kitu ambacho ni kweli kabisa, ukiangalia maeneo ya strong hold za CCM utakuta ni yale maeneo ya low literacy level na stinking povery!, maeneo ambayo wameweza kuchagua wapinzani ni yale maeneo yenya angalau kielimu elimu na hali bora kiuchumi, exception kwa huku bara ni Lindi, na upinzani ulichaguliwa kwa kura za sympathetic votes!, naamini unanielewa!. Nisome hapa chini mimi nilivyolizungumzia
 

Ukipata muda hebu sikiliza hii mihadhara kuhusu democracy, maendeleo na elimu
https://www.ted.com/talks/eric_x_li_a_tale_of_two_political_systems
https://www.ted.com/talks/dambisa_moyo_is_china_the_new_idol_for_emerging_economies
https://www.ted.com/talks/bill_gates_unplugged
kwa maoni yangu umaskini na ujinga ndiyo mtaji wa CCM, japo inawezekana baada ya kipindi kirefu cha msoto maskini sisi tunaweza pata "true consciousness" as opposed to "false consciousness" (as per Karl Marx) and evict CCM kupitia mapinduzi/#sanduku la kura??...Hivyo basi tusichoke kuwaelimisha wenzetu kwani ipo siku tu!
 

Naendelea kufanya tafakuri za niliwahi kusema nini na sasa kinatokea nini, uzi huu niliupandisha mwezi Aprili 2014, nikiupa upinzani possibility ya 2020!, lakini ujio wa Lowassa Chadema, ume change scope yote, hivyo sasa CCM inampasukia rasmi JK mkononi kwake na upinzani unatinga ikulu 2015!. Kifo cha CCM sio kwa Lowassa kujiondoa na kujiunga Chadema, pale kazi ya kwanza ya serikali mpya ya upinzani ikiishaingia madarakani, utaifanya nini CCM!.

Pasco
 
Nadhani ilo lipo wazi maana lowassa ndo chaguo la wengi badara ya kubembeleza ndoa jk kaamua kuvuruga kila kitu sasa wakat ni huu watu wajiandikishe kwa wingi ili wachague ukawa
 
Najikumbusha tuu na kutafakari kwa muktadha wa hiki kinachoendelea Zanzibar!.

Pasco
 
Mkuu Salary Slip, natafakari tuu!.

Pasco
https://www.jamiiforums.com/member.php?u=84376
 
Leo ni Sikukuu ya Muungano, nachukua fursa hii kuutafakari Muungano wetu adhimu, kupitia hoja mbalimbali za kimuungano.

Nawatakia maadhimisho mema ya muungano na mapumziko mema.
P
 
Hiki ni kipindi ambacho Pascal aliitwa Pasco, ndio alikuwa hivi sasa. Na ni miongoni mwa watu wachache sana walionivutia kujiunga JF. Kwa bahati mbaya siku hizi nikijaribu kusoma hata paragraph ya mwanzo tu ya maandiko yake nakosa kabisa mood ya kuendelea kusoma.

Alivyokuwa Pascal Mayala akawa mtu mwingine kabisa. Siku hizi kazi kubwa yeye ni kuleta maandiko yenye mlengo wa kuishambulia CHADEMA na viongozi wake. Si bure, nadhani kuna mahali walikosana ndio maana akaamua kubadili kabisa fikra zake na kuwa mtu wa hoja nyepesi nyepesi na si kama kipindi kile. Kwa bahati mbaya kwa sasa ukimwambia kuwa kabadili gia atakushushia links nyiiiingiiii za maandiko na kusema sisi ndio wenye mtizamo hafifu ila yeye yupo sawasaa. Maisha ndivyo yalivyo. Binadamu hubadilika.
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…