Chonde chonde Rais Samia mkumbuke Mwijaku katika uteuzi

Lady Mwali

Senior Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
147
Reaction score
333
Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Naomba umteue mtangazaji wa Clouds FM katika cheo cha ukuu wa wilaya kwani kijana huyu ni mzalendo wa hali ya juu.

Kuchukua fomu ya kugombea cheo cha Spika hivi leo kumeonesha jinsi gani Mwijaku ana nia ya kuwatumikia Watanzania.

Mara zote kijana huyu amekuwa mstari wa mbele kuonesha uchawa wa hali ya juu kwako.

Ni mtangazaji wa Kwanza kutangaza kwamba yeye ni chawa wako, na yeyote anayekupinga atapambana naye. Mh.Rais huoni kwamba huyu kijana amejitolea maisha yake kwa ajili yako bila kujali hatari ya Sukuma Gang ya kumzulu?

Isitoshe huyu kijana ni msomi ana degree mbili kutoka vyuo viwili tofauti,UDSM na MZUMBE.

Naomba sana mtukufu Rais kwenye teuzi zako usimsahau,
natabili Mwijaku atagombania hata Ubunge kupitia CCM 2025, akipata mteua awe hata naibu waziri.

Ni hayo tu.
 
Unafikiri vyeo vinagawiwa kama njugu?
 
Akili shida sana
 
Mwijaku ni ushamba unamsumbua na kutafuta kikck za kijinga.
 
Mbona hukuwahi kumuombea Musiba kipindi cha Jiwe maana alijitolea kuoambana na yeyote ambaye angempinga Jiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…