May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kutokana na kuwa Simba wanaendelea kupata matokeo mazuri kumekuwa na kelele kila kona kutoka kwa Mashabiki wakitaka Mgunda apewe timu kamili kama Kocha Mkuu.
Na Viongozi wa Simba ni kama vile wamekaa wakisubiri kama vile wanasikilizia. Nadhani hili litawagharimu Simba, huu mchezo wa kuwafuatisha Mashabiki sidhani kama utakuwa na mwisho mwema.
Ninashauri Simba waendelee na wakamilishe mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu na Mgunda na Matola wabaki kama Wasaidizi wakiendelea kupata uzoefu, walau kwa misimu miwili.
Shughuli iliyopo mbele bado ni mzigo mkubwa kwa Mgunda na Matola na inavyoonekana matokeo mazuri wanayoyapata Simba pamoja na maelekezo ya mwalimu ila ni kama pia kuna morali binafsi ya wachezaji, na hili halitachukua muda mrefu.
Namuheshimu sana Mgunda, lakini kutoka Coast mpaka Simba na kuridhika na matokeo yanayopatikana ni kucheza kamari tu.
Kama ni kweli kulikuwa na mpango wa kumfuatilia Kocha wa Asec basi mipango hiyo ifanyike ikiwezekana Kocha aje.
Mashabiki wenu hawa timu itakapoanza kukosa matokeo kama kawaida watabadilisha kiitikio(chorus) na hamtokuwa tayari kusikiliza nyimbo zao.