Chonde chonde Viongozi Simba msimtwishe Mgunda zigo zito, mtamuumiza

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kutokana na kuwa Simba wanaendelea kupata matokeo mazuri kumekuwa na kelele kila kona kutoka kwa Mashabiki wakitaka Mgunda apewe timu kamili kama Kocha Mkuu.

Na Viongozi wa Simba ni kama vile wamekaa wakisubiri kama vile wanasikilizia. Nadhani hili litawagharimu Simba, huu mchezo wa kuwafuatisha Mashabiki sidhani kama utakuwa na mwisho mwema.

Ninashauri Simba waendelee na wakamilishe mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu na Mgunda na Matola wabaki kama Wasaidizi wakiendelea kupata uzoefu, walau kwa misimu miwili.

Shughuli iliyopo mbele bado ni mzigo mkubwa kwa Mgunda na Matola na inavyoonekana matokeo mazuri wanayoyapata Simba pamoja na maelekezo ya mwalimu ila ni kama pia kuna morali binafsi ya wachezaji, na hili halitachukua muda mrefu.

Namuheshimu sana Mgunda, lakini kutoka Coast mpaka Simba na kuridhika na matokeo yanayopatikana ni kucheza kamari tu.

Kama ni kweli kulikuwa na mpango wa kumfuatilia Kocha wa Asec basi mipango hiyo ifanyike ikiwezekana Kocha aje.

Mashabiki wenu hawa timu itakapoanza kukosa matokeo kama kawaida watabadilisha kiitikio(chorus) na hamtokuwa tayari kusikiliza nyimbo zao.
 
Wacha Mgunda apige job hapo bwana mbona mnataka makocha wa kidhungu waje tuu huku kwetu wakati wao huko kwao hawatutaki. Tuache ujinga wacha apewe timu. Exprience ataipata huko huko anavyoenda.

Tumekalia kuwapa foreigners matimu tunakuza CV zao tu wakati wazawa wanasaga meno tu. Wacha Pep Mnene aende makundi bwana.
 
Hiyo haiondoi ukweli kuwa ni kucheza kamari.

Guadiola akikaa walau msimu mmoja au miwili atakuwa amekomaa..kutoka Coast kuja Simba sio cvb inayotosha.
 
Hiyo haiondoi ukweli kuwa ni kucheza kamari.

Guadiola akikaa walau msimu mmoja au miwili atakuwa amekomaa..kutoka Coast kuja Simba sio cvb inayotosha.
Sasa sii bora kamari hiyo kuliko kamari za wadhungu alafu hamna kitu. Tumedanga ywa hapa mtu katoka madrid yaani pira litapigwa mpaka mshangae....tukaishia kuanza kisema alikuwa mtunza vifaa wa real madrid 🤣🤣🤣🤣

Its a risk yes, but so is any other appointment of a coach ukizingatia simba wenyewe wagwadu tuu hawataki makocha wakubwa wenye kiwez kufika semi au final maana hao wanataka kuja na wasaidizi wao.
 
Haya ni mawazo mgando. Wazungu hata Mosimane hawajataka kumchukua pamoja na mafanikio makubwa. Aachiwe timu Mgunda maana akifanikiwa hapo anaweza kuwa mwanzo wa makocha wetu kupewa timu za kimataifa.
Bora wee umeongea ukweli. Mosimane hawajamkubali pamoja na mafanikio yake yote hayo. Waafrica tunapaswa kuendesha club zetu wenyewe.
 
Swali, Kati ya kocha mzawa na mgeni yupi anaujua mpira wetu?
Wabongo wengi hatuaminiani, lkn pia tumejawa na roho za husda hatupendi wengine wapate.

Sina maana J. M apewe timu, ila hebu tuwaamini na tujiamini pia.

Sent from my LDN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli Mzawa anajua lakini hupotezi kitu kwa kuendelea kupata uzoefu kutoka kwa waliotutangulia kisoka.

Akipatikana Kocha mwenye CV zilizoshiba atakuwa Mentor mzuri tu kwa Mgunda na Matola, hasa kwa mustakabali wao huko mbeleni.
 
Ngoja kwanza tuweke mambo sawa. Kocha yoyote yule mzuri na unampa project ya kukufikisha semi final au final atakuja na watu wake. Hawezi kuja yeye kama yeye. Cha pili kocha wa ukweli ni gharama boss, not less than $30,000 huo ndio ukweli boss.
Angalia mosimane ana timu yake ya watu wawili anaoenda nao. Kuna fitness trainer na kuna opposition analyst.
 
Hivi unaelewa ulichoandika? unaishi kama mwanamke aisee! kiherehere kama mkojo wa asubuhi!
 
Tumwamini ttu kama tunavowaamini wazungu!.... Wazungu wenyewe wababaishaji tyu!
 
 
Ni bora kushika kidogo ulichonacho kuliko ahadi ya kupata kizuri kisicho na uhakika.
Ni bora kamari ya Mgunda ambae anaendelea vema kwasasa kuliko huyo ajae hatujui kama ataendeleza mazuri ya sasa au ataaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…