Serikali futeni kesi zote zenye mlengo wa kisiasa hasa ya Mbowe na Sabaya
1. Msilazimishe watu kuchanja chanjo ya UVIKO-19 kwa vitisho
2. Mwendesha mashitaka futa mashitaka dhidi ya Mbowe na Sabaya ili kuiponya nchi na BALAA linalokuja
3. Utawala uliopo usidhalilishe viongozi walio chini yao kwa kufungulia mashitaka ya visasi na chuki
4. Askari polisi waache dhuluma, kusingizia kesi na kufanya visasi dhidi ya wananchi wanaotoa siri ya udhaifu wao
5. Wanasiasa wasameheane hadharani kwa kushirikisha wananchi kisha wajenge nchi kwa pamoja
6. Viongozi mliopo madarakani acheni kudhalilisha viongozi wa nchi waliotangulia mtaharibikiwa vibaya sana
7. Mamlaka ya nchi iache kuingilia viongozi wa kidini na kiroho, maombi ya WIKI moja yaridhiwe na nchi kwa pamoja
8. Tanzania iko kwenye hatari ya kuvamiwa kwa sasa, wananchi, jeshi la ulinzi, uongozi wa nchi na viongozi wa dini/kiroho unganeni haraka muachane na ubishi wa mabavu ya mamlaka
9. Jeshi la polisi lindeni raia na mali zao
10. Tekelezeni miradi yote ambayo wanasiasa mliahidi kwenye uchaguzi mkichepusha kuna somo lipo mezani kuifundisha Tanzania
11. Vyama vya siasa muwasamehe CCM kwa yote mnaodhani waliwakwaza; ninyi CCM mjishushe muache kiburi mtasambaratika ijapokuwa hilo huwa hamuliamini lakini litatokea hakika
12. Mamlaka ya nchi acheni kuwabebesha mzigo wa kodi wananchi wa chini hii laana itaangusha utawala wenu
13. Tamkeni hadharani kama makao makuu ya nchi yamehamishwa kutoka Dodoma kurudi Dar Es Salaam ili wananchi waelewe na kuridhia au la tofauti na hapo kuna mvutano utaleta athari kwa uchumi. usalama na jamii itaparaganyika
14. Viongozi mlioko madarakani na wanasiasa ama wa chama tawala au upinzani jiepusheni kumtupia lawama hayati JPM kwa lolote lile ili mpendwe haitatokea, na amani itarejea mkiwa na moyo wa kusamehe na kuanza upya kila mmoja akimheshimu mwingine
15. Safari za nje ya zisizo na tija zisitishwe na viongozi watatue kero za wananchi wa chini hapo mtapata kibali bila hivyo utawala unaonekana kutoendela kusisima
16. Aina ya utatuzi wa kero za muungano unaoendelea usitishwe na wananchi washirikishwe watawashauri vizuri tu kwa manufaa ya pande mbili maana kuna fukuto miongoni mwenu....................kwa maana inaonekana minong'ono ya kutotendewa haki kila upande inafukuta kila upande ukilaumu upande mwingine, Kumbukeni Tanzania imejengwa kwa tofali za chuma kichafu na udongo wa mboji kwa hiyo mtikisiko pasipokuwa na mahusiano mazuri, kuaminiana, kusaidiana, kujengana na kuheshimiana kutaipasua vipande (Zanzibar vipande sita Pemba viwili, Unguja vinne) Tanzania bara (vipande saba Kasikazini, Kasikazini Magharibi, Pwani, Nyanda za juu kusini, Kusini, Kati na Magharibi)
*Watumishi wa Mungu, Wananchi wa chini, Vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa waandamizi wa nchi WAHESHIMIWA, WASAIDIWE, nao waondoe KIBURI giza linaweza kupungua