Chonde chonde wastaafu wenzangu, NSSF, PSSSF, nk.

Chonde chonde wastaafu wenzangu, NSSF, PSSSF, nk.

Ni muhimu kujuzana, maana ukisinzia kidogo tayari wanakula kichwa.
 
Tafadhali sana tujuzane tarehe za kuhakiki, ni January hii.
Tusije tukafutwa kwenye vipension vyetu!!
Kwa PSSSF kila mstaafu ana tarehe tofauti ya kuhakiki. Kama unapaswa kuhakiki mwezi February ukaenda kuhakiki January uhakiki wako ni batili.
Kama kama ulipaswa kuhakiki January na ukaacha kwenda kwa sababu mbalimbali tuseme ukaenda kuhakiki mwezi July basi utalipwa pensheni yako ya kuanzia January.
Ni vyema kufuatilia ili kujua tarehe halisi ya kuhakiki. Sio lazima iwe January.
 
Asante sana Mkuu!
 
Kila mstaafu anapangiwa mwezi wa kuhakikiwa. Mimi nimepangiwa kuhakikiwa tangu tarehe 10.1.2022.
 
Ule mwezi uliohakikiwa mwaka jana ndiyo unakuwa mwezi wako wa kuhakikiwa kila mwaka. Mimi nilienda ofisini mwao na kuona tangazo la uhakiki kwa mwezi Januari, 2022.
 
Mkuu, leo nimepata SMS, natakiwa niende tarehe 25/01/2020.
Asante sana kwa ushirikiano
 
malipo yakoje yakoje? Yanarange vipi? Au ndio siri ya chama?
 
Daah ndio maana huwa na reply post kwa umakini sana, vijana humu ndani jipeni walau 3 to 6 seconds kabla huja click post reply.
 
Hongereni kwa hatua kubwa ambayo vijana wa sasa ni ngumu kuifikia
 
Back
Top Bottom