kujitambua ni hatua ya kwanza kuelekea kupata suluhu.
kama bado tunadhani wakati wa kampeni unapofika kila mmoja wetu atafute mgombea wa kumsapoti ili baada ya uchaguzi kukamilika kama karata yake ameicheza vizuri basi anapata angalau nafasi kuteuliwa katika nafasi alizopewa raisi kufanya uteuzi au kuingizwa nafasi nzuri.
hakuna anayehoji hawa watatufanyia nini ili tuwachambue tupate the best among them badala yake tunasapoti hata ujinga ulioko katika makundi yetu na kukosoa ukweli ulioko kwenye makundi tofauti na yetu.
tunawachanganya wananchi kiasi hawajui wachague kwa kutumia kigezo gani maana kila mgombea ana wanaomsema vibaya na wanaomsema vizuri. tumejikuta uzuri wa mgombea au ubaya wake si hoja tena bali ngonjera na katika ngonjera sidhani kama tunaweza kupata kiongozi mzuri.
lakini yote haya yanachagizwa na makundi ambayo yanajengwa nyuma ya wagombea kwani ndani ya hawa wapo wanaotafuta nafasi za kimaslahi hivyo hata kama anayemsapoti anaona kabisa huyu anatumia "gear" ya "riverse" na akipita taifa haliwezi kupiga hatua yoyote lakini kwake yeye binafsi huyo akipita ndiye anaweza kumpa nafasi mfano apewe ukurugenzi wa shirika wakati hana uwezo wa kuliongoza akalifilisi kwa uongozi mbaya na dili za kuliibia ilimradi atengeneze maisha yake mwenye.
majority yetu ni bendera ambazo hazitathmini tunayoelezwa ili mwisho wa siku tupate kiongozi bora kutokana na yanayotukabili bali upepo ukivuma kuelekea huku basi tunafuata.
ujinga huu wa kufikiri ni hatari sana na anayefanya uchaguzi katika ujinga bila kuelewa mantiki ya kile anachokifanya bali kubeba taswila nyingine na kuanza kufanya upuuzi akidhani ndio anapata kumbe anapotea huwezi kusema anafanya uchaguzi wa kidemokrasia.