Uchaguzi 2020 Chondechonde Vyama vya Upinzani, waacheni Wabunge waliochaguliwa na Viti Maalum wakatuwakilishe

Uchaguzi 2020 Chondechonde Vyama vya Upinzani, waacheni Wabunge waliochaguliwa na Viti Maalum wakatuwakilishe

Tunguja

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2018
Posts
457
Reaction score
339
Mkiwazuia hao mtetezi wetu atakuwa nani kule bungeni?

Muendelee kupigania haki za waliodhurumiwa wakati waliopewa haki wakiendelea kutuwakilisha, vinginevyo sisi tutakuwa wakiwa hatutakuwa na mtetezi.

Kama mjuavyo wale wa upande wa pili hawatakuwa na uwezo wa kuhoji lolote zaidi ya kuunga mkono na kupongeza hata kama halitakuwa na maslahi kwetu sisi wanyoge, hilo ni ombi ila mkifanya tofauti nitaandamana peke yangu.
 
Mkiwazuia hao mtetezi wetu atakuwa nani kule bungeni? Muendelee kupigania haki za waliodhulmiwa wakati waliopewa haki wakiendelea kutuwakilisha, vinginevyo sisi tutakuwa wakiwa hatutakuwa na mtetezi...
Bunge hili ambalo hotuba za upinzani zinafanyiwa editing na ofisi ya Spika?

Hakuna haja, amesema Msekwa, wapinzani walikuwa na kelele. Waachiwe bunge lao.
 
Mkiwazuia hao mtetezi wetu atakuwa nani kule bungeni? Muendelee kupigania haki za waliodhulmiwa wakati waliopewa haki wakiendelea kutuwakilisha, vinginevyo sisi tutakuwa wakiwa hatutakuwa na mtetezi...
Tatizo ni wachache sana, Mbowe Hana faida nao Tena maana aliwakata mishahara michango haitunishi mfuko wa chadema.
 
CHADEMA wakigoma, CCM wanaweza kufanya lolote ikiwemo kubadilisha utaratibu haraka ili kuwapa hizo nafasi TLP au ‘mpinzani’ fake mwingine yeyote yule na ikawa hasara kwa Taifa double double.

Kumbuka kuna kamati mbili za mambo ya Fedha lazima ziongozwe na Wapinzani na CCM bila shaka watahakikisha hilo linatendeka

Viti maalumu plus hao wawili inaweza kuwa wabunge 18 hivi. Something is better than nothing na wakati mwingine ni sawa kuswallow pride ili kujipanga upya kama Taasisi
 
expand...
Kikao cha kususia Bunge kilipofanyika hakukuwa na mwanamke hata mmoja. Kwahiyo huu ni mfumo dume unaodharau nafasi ya wanawake kujiamulia mambo yao wenyewe.

Haikuwa Sahihi kutangaza uamuzi bila kuwashirikisha kinamama wenyewe.
 
Mimi nasema waende ili wakale hela kwakuwa maisha ni magumu, lakini sioni lolote la maana humo ndani. Kwangu mimi hilo bunge ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
tindo,
Wewe ni miongoni mwa GT wa JF nakuheshimu sana. Uamzi wa kwenda bungeni Wabunge walitangazwa ni uamzi sahihi kwa sababu zifuatazo;
1.Wabunge hao hawakutangazwa kama hisani bali wamepambana na dhuluma hadi kutangazwa baada ya kuganikiwa kuzuia kuingizwa kura feki vituoni.

3.Wasimamizi wa Uchaguzi wa maeneo hayo wameongozwa na Utu na ucha Mungu na kuamua kuacha udhalimu na kutenda haki hivyo si sahihi kuwakatisha tamaa watumishi walioamua kumheshimu Mungu na kutenda haki.

3.Waliotangazwa hawakufanyiwa hivyo ili kupumbaza Dunia kwamba kuna demokrasia Tanzania. CCM walikuwa wameamua kunyang'anya kila kitu isipokuwa pale iliposhindikana.
 
Lakini mnaona wabunge wote wa upinzani walipshiriki walishinda?

Na wameshinda ila wamenyang'aywa ubunge wao ?

Tumewahi kushinda viti vyote vya bunge ambapo tuliweka wabunge washindane ?
 
CHADEMA wakigoma, CCM wanaweza kuwapa hizo nafasi TLP au ‘mpinzani’ fake mwingine yeyote yule na ikawa hasara kwa Taifa double double

Viti maalumu plus hao wawili inaweza kuwa wabunge 18 hivi. Something is better than nothing na wakati mwingine ni sawa kuswallow pride ili kujipanga upya kama Taasisi
Katiba inasema chama kipate angalau 5% ndipo kinapata wabunge wa viti maalumu. Idadi itategemea na % ilichopata juu ya 5%. Hivyo vingine havijafika hiyo minimum requirement, labda kama utamaduni wenu wa kukanyaga katiba ukitumika.
 
Naona wao waliochaguliwa waendelee na shuguri za wananchi. Ni bora hao 18 kuliko kuwa bila hata moja ndani ya mjengo.
Kumbe upinzani ni wa muhimu mjengoni!??. Siyo wanaturudisha nyuma!?
 
Wakigoma watakuwa wamedhulumu haki ya wapiga kura waliowachagua sawa na CCM waliodhulumu haki ya wapiga kura kupitia kura fake.
Wananchi wamemsikia aliyesema wasimchanganyie, anataka wachague kijani tu awaletee maendeleo. Nani asiyependa maendeleo. Tunasubiri maendeleo, usitutingishe mkuu. Tunataka tukajadili maendeleo Bungeni.
 
tindo,
Wewe ni miongoni mwa GT wa JF nakuheshimu sana. Uamzi wa kwenda bungeni Wabunge walitangazwa ni uamzi sahihi kwa sababu zifuatazo;
1.Wabunge hao hawakutangazwa kama hisani bali wamepambana na dhuluma hadi kutangazwa baada ya kuganikiwa kuzuia kuingizwa kura feki vituoni.

3.Wasimamizi wa Uchaguzi wa maeneo hayo wameongozwa na Utu na ucha Mungu na kuamua kuacha udhalimu na kutenda haki hivyo si sahihi kuwakatisha tamaa watumishi walioamua kumheshimu Mungu na kutenda haki.

3.Waliotangazwa hawakufanyiwa hivyo ili kupumbaza Dunia kwamba kuna demokrasia Tanzania. CCM walikuwa wameamua kunyang'anya kila kitu isipokuwa pale iliposhindikana.
Safari hii hakuna mahali eti CHADEMA wamepambana. Waliotangazwa kushinda ni mpango maalum na kwa malengo maalum. Ni Magu anaeamua nani awe mbunge na yupi aachwe
 
Lakini mnaona wabunge wote wa upinzani walipshiriki walishinda?

Na wameshinda ila wamenyang'aywa ubunge wao ?

Tumewahi kushinda viti vyote vya bunge ambapo tuliweka wabunge washindane ?
Siyo hivyo. Hata wewe unawajua wa kushinda ni wapi. Hata hao wa kushinda siyo lazima wote, lakini si kwa hali tuliyofikishwa sasa. Ona sasa, watu wanaanza kuomba hata hawa wachache wasikosekane Bungeni. Aliyekua anasema hataki kuchanganyiwa hakujua kwamba mnapenda upinzani uwepo.
 
Wewe maandamano tu,bila shaka utakuwa umetumwa
 
Nafasi ya viti maalum hawana, ni kama zito alivyo kuwa bungeni mwenyewe hakuwa na viti maalum, na saivi CDM hawana tofauti na yule mmoja sijui 3.
 
Nafasi ya viti maalum hawana, ni kama zito alivyo kuwa bungeni mwenyewe hakuwa na viti maalum, na saivi CDM hawana tofauti na yule mmoja sijui 3.
Chadema wana qualify kupata wabunge wa viti maalumu. Requirement ni kura za wabunge zifike at least 5% na chadema wamefika na kuzidi. Idadi inategemea na % juu ya hiyo 5%.
 
Back
Top Bottom