JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Chongolo aliyasema hayo wilayani Iramba akiwa katika ziara ya siku sita mkoani Singida akifuatana na Sekretarieti ya CCM kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 na kuzungumza na wananchi. “Wapo baadhi ya watu wanakaza nyuso na shingo zao kutaka kuonesha nchi hii inakopa sana, niwaambie tu katika nchi za Afrika Mashariki, nchi ambayo haina mzigo wa mikopo kuliko zingine zote ni Tanzania,” alisema Katibu Mkuu wa CCM.
Chongolo alisema hakuna nchi duniani ambayo haikopi, akitoa mfano kuwa hivi karibuni Marekani ilikopa kwa China ili mambo yake yatatuliwe. “Wote mnajua Marekani ndo dunia nyingine, nendeni mkaangalie mjiridhishe mimi ni kiongozi mkuu wa chama siwezi danganya, nimetaja kwa jina kwa sababu ni ukweli, hapa kuna mtu hajui kukopa? Kuna mtu amewahi kufa kwa kukopa?” Alihoji Chongolo. Alisema mtu asiyetaka maendeleo hutengeneza mazingira ya kujifunga kama kisiwa na kusisitiza nchi zote zinakopa.
Chanzo: HabariLEO