A
Anonymous
Guest
Choo kilichopo kina vyumba viwili, kimoja ambacho kipo wazi kwa ajili ya Wananchi kutumia ni kichafu kipo katika hali ambayo sio salama kiafya.
Ndani ya choo hicho hakuna miundombinu rafiki ya maji, mazingira hayo yanatuweka katika mazingira hatarishi zaidi ya kupata magonjwa.
Kutokana na hali hiyo kukumbana nayo kwenye kituo hicho mara kwa mara sina budi kuziomba mamlaka za kiafya kufuatilia mazingira ya choo hicho kwa kuwa kinahatarisha afya za Wananchi wengi wanaofika kituoni hapo.
Sio jambo jema ofisi ya umma kama Polisi ambayo inapokea watu wengi tena kwa muda wa saa 24 kukosa miundombinu bora ya vyoo. Binafsi nilitegemea wawe mfano bora kwa jamii katika kuzingatia mazingira ya kiafya.