KERO Choo cha Umma Kituo cha Polisi Kawe (Dar) sio salama Kiafya kwa Watumiaji, miundombinu yake sio rafiki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest

Mara kadhaa nimefika Kituo cha Polisi Kawe kwa ajili masuala mbalimbali lakini nasikitika kusema kwamba watu ambao tunafika kituoni hapo tunakumbana na changamoto ya huduma choo ambayo sio rafiki.

Choo kilichopo kina vyumba viwili, kimoja ambacho kipo wazi kwa ajili ya Wananchi kutumia ni kichafu kipo katika hali ambayo sio salama kiafya.

Ndani ya choo hicho hakuna miundombinu rafiki ya maji, mazingira hayo yanatuweka katika mazingira hatarishi zaidi ya kupata magonjwa.
Hata hivyo ukiomba ufunguo kwenda kwenye choo kingine ambacho kinakaa kimefungwa wanakuwa wagumu, wanachagua nani wampatie funguo.

Kutokana na hali hiyo kukumbana nayo kwenye kituo hicho mara kwa mara sina budi kuziomba mamlaka za kiafya kufuatilia mazingira ya choo hicho kwa kuwa kinahatarisha afya za Wananchi wengi wanaofika kituoni hapo.

Sio jambo jema ofisi ya umma kama Polisi ambayo inapokea watu wengi tena kwa muda wa saa 24 kukosa miundombinu bora ya vyoo. Binafsi nilitegemea wawe mfano bora kwa jamii katika kuzingatia mazingira ya kiafya.



 
Duh,hatari sana, mkuu wa kituo ni nani hapo!
 
Tanzania bado hatujastaarabika. Itachukua miaka mingi
 
Sasa kama ni hivyo ni bora mrudi tu kwenye vichaka na kuchamba kwa majani
Hakuna cha polisi wala nini kila sehemu public toilet ni balaa
Na sio vyoo tu hata misingi na majalala ni hali moja tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…