Choo ni kipimo cha ustaarabu katika jamii

Kipindi Niko TANGA miaka hiyo nakaa chumba Cha kupanga. Nyumba Safi, toilet Safi japo Ni Shimo i.e Swahili type. Kuna dogo akiona kaja mgeni na anataka amtoe mgeni nishai anakwenda kuchafua chooni. Mama mwenye nyumba akienda kuona huo uchafuzi si unajua wadigo walivyo, hawezi kumezea. Lazima ataliweka wazi Tena kwa sauti ya juu. " Kwamba humu ndani choo chetu siku zote Ni kisafi, huyo aliuekichafua lazima atakua huyo mgeni wa mpangaji x, mpangaji x naomba ukafanye usafi chooni, mgeni wako kaharibu"
Kesho yake hutamuona huyo mgeni .
 

Umenikumbusha S.Africa ndipo nikagundua kuwa ustaarabu wa mwafrika nenda chooni ndio utajua kuwa yupo vipi.sehemu ambapo waafrika wapo tena wale akili china unaweza kutapika,ukiwa kwa ngozi nyeupe unaweza tamani kula hapo chooni maana usafi
Wa nguvu kabisa.
 
Ni kweli kabisa, choo cha mstaarabu kina mpaka maua, magazeti, unaweza kukaa na kusoma gazeti. Na kabla hajatoka anahakikisha amekuacha katika hali nzuri.
 
Upo sahihih sana. Kuna kipindi miaka ya zamani 2000s tuliwahi kupanga katika nyumba moja iliyokuwa na choo kibovu sana maeneo ya Kurasini. Ilikuwa mtu mmoja akitoka kuoga ni lazima mwingine ayafagie yale maji kama dakika tano ndio uingie kuoga, mpaka ndugu wakawa wanaogopa kuja kutusalimia. Daaah, ile changamoto sitakaa niisahau.

By the way, siku hizi vyoo vingi vya shimo huku uswahilini kwetu wamevifanyia modifications na kuweka hizi european styles kiasi kwamba mtu akiwa anajihudumuia hawezi kupata kadhia ya harufu ya taka ngumu au kutunza wadudu kama mende pamoja na mbu.

All in all, uzuri wa nyumba ni choo, literally.
 
Hasa wanawake kazini wanajifanya hawawezi kukalia kiti mpaka waweke tissues, anaacha tissues zimeanguka sakafuni na choo hasafishi.
Binafsi sidhani kama choo cha kukaa ni sahihi kwa matumizi ya umma kama vile ofisini. Choo cha namna hiyo kikiwepo huko master bedroom kwa ajili ya mke na mume ni sahihi zaidi kuliko kwenye public.
 
Binafsi sidhani kama choo cha kukaa ni sahihi kwa matumizi ya umma kama vile ofisini. Choo cha namna hiyo kikiwepo huko master bedroom kwa ajili ya mke na mume ni sahihi zaidi kuliko kwenye public.
Vyoo vya kuchuchumaa ni changamoto kwa wenye umri mkubwa 70+. Lakini choo cha kuchuchuma hata mimi sikipendi. Ila ni rahisi kwa wageni wakati una choo cha kukaa master bedroom.
 
Nilienda sehemu moja jamaa kawekeza sana sehemu nzuri ya kula... Bites, snacks, vinywaji safi, muziki wa maana, misosi sana, kuku choma, samaki Choma, n.k...

Lakini nivyoenda chooni... Nikakasirika.... Choo kilikuwa kichafu hakilingani na uwekezaji alioufanya....

Uchafuu umejaa hadi juu,.... Hovyo kabisa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…