Crosby
Member
- Aug 25, 2022
- 5
- 3
Msomi ni mtu aliyemaliza elimu ya chuo kikuu kuanzia walau degree moja. Tunapozungumzia msomi ni mtu ambaye ameandaliwa ili aweze kutatua changamoto za jamii kutumia elimu yake aliyo ipata shuleni. Kila mwaka idadi ya wasomi nchini inazidi kuongezeka, hii upelekea kuwa na wasomi wengi nchini.

Chozi ni neno lililo beba nadharia ya mambo magumu ambayo msomi wa kitanzania anayapitia kipindi anatafuta elimu yake na baada ya kupata elimu.
Je, wasomi hao wakimaliza vyuo vikuu huenda wap? ili kuweza kutumia elimu yao waliyo ipata. Hapa ndo “CHOZI LA MSOMI” linaibuka. Chozi la msomi linaweza likawa katika makundi mawili, akiwa anatafuta elimu na baada ya kumaliza elimu ya chuo kikuu tuziangalie kama ifuatavyo:
I: CHOZI AKIWA ANATAFUTA ELIMU
Hapa ujumlisha mambo yote ya msomi anayopitia kipindi anatafuta elimu yake . Hapa tutaangalia hayo machozi ya msomi, kama ifuatavyo;
Kumalizia kwa kusema Serikali inabidi iingilie kati ili kuweza kuangalia mtaala wa elimu ya kitanzania ili uweze kubadilishwa kuendana na uhalisia wa mtaani.Hii itasaidia kuwaanda wasomi kuweza kuendana na mazingira ya sasa (sayansi na teknolojia), kwani mtaala uliopo ulikua kwa ajiri ya miaka hiyo ya sabini (azimio la viwanda) kuwaanda kuwaanda ili wakaajiriwe.
Kingine inabidi mwanafunzi binafsi kujiongeza kipindi anakuepo chuo, kufikiria nje ya boksi kama Mh. Hamisi Kigwangala anavyosema.
Asante!

- Matumizi ya lugha mbili (Kiswahili na Kiingreza) , unakuta mtu kamaliza elimu yake ya msingi, ambapo lugha ya kufundishia ni Kiswahili, anapo ingia secondari lugha ya kufundishia inabadilika kuwa kiingreza. Sasa hichi kitendo kinafanya elimu kuwa ngumu kwa wanafunzi. Sasa hapa mwanafunzi itabidi aingie chozi ili kuweza kuelewa mambo anayofundishwa mashuleni ili kuweza kuendana na kiingereza. Sasa hichi kitendo pia hupunguza ufanisi wa elimu yetu. Kwani Kiswahili pia kinaweza kikatumika katika kupata elimu.
- Kusoma vitu vingi ambavyo havina uhalisia na maisha ya mtaani, hichi ni kitendo cha mwanafunzi kusoma vitu vingi ambavyo havina umuhimu sanaa katika uhalisia wa maisha ya mtaani, kwani ni kumbebesha mzingo mzito sana usio wa lazima. Hii huonekana pale ambapo wasomi wakikosa kazi inabidi waanza upya kujifunza jinsi kitaa kinavyo fanya kazi (elimu ya kitaa).
- Kusoma kwa mateso kisa uhaba wa walimu, kwa watu waliosoma shule binafsi (PRIVATE) awawezi kunielewa na maanisha nini. Na idadi kubwa ya wasomi wamesoma shule za serikari. Hapa unakuta baadhi ya masomo unakuta hayana walimu sasa hii hupelekea mwanafunzi binafsi kupambana kutafuta njia mbadala ili aweze kufanya vzuri hayo masomo ambayo hayana walimu.
- Kusomeshwa kwa gharama kubwa, Wazazi au walezi wanahangaika sana kuwasomesha watoto wao kwa gharama kubwa mno. Sasa hii inapelekea kuwa na chozi au maumivu kwa wazazi pamoja na Watoto wao wanao wasomesha. Chozi wanalopata wazazi kutafuta ad ani kubwa sana hasa ifikapo mwezi januari unaweza ukawaonea wazazi huruma.
- Kusoma masomo mengi, hichi ni kitendo cha mwanafunzi kusoma vitu vingi ambavyo vingine hata vitumia baada ya kumaliza masomo yake. Kama mtu anapenda kuwa mhandisi au daktari kwanini asianze kuwa mbobevu mapema. Hichi kitendo kitamfanya kuwa mtata katika taaluma yake na kuongeza ufanisi katika kazi. Inatakiwa mwanafunzi asome vitu vyenye umuhimu kwani ufanisi uongezeka na kuwa mbobevu.
- Ukosefu wa Ajira, Hili ni tatizo kubwa kwa sasa linalo ikumba nchi yetu ya Tanzania. Tatizo limekuwa gumu linaikumba kila idara iwe afya, ualimu, elimu au uhandisi. Sasa hapa wasomi wengi wanamwaga machozi mazito. Sasa hapa wasomi wengi wanamwaga machozi mazito. Sasa hii inafanya kuongezeka kwa wasomi wengi mtaani wakiwa wanashinda vijiweni. Sio tu msomi kumwaga machozi hata wazazi pia, uku wakijutia gharama kubwaa walizo zitumia kumsomesha mtoto wao.Kushinda vijiweni kinaweza kuzalisha panya road zaidi au matukio mengi ya uwalifu ili waweze kupata chochote cha kujikimu.
- Elimu kutokuendana na maisha ya mtaani, sasa hapa ndipo anagundua elimu aliyo ipata takribani miaka kumi na sita haina uhalisia wa mtaani. Sasa hapa, inamfanya msomi kuanza upya tena kusoma na kudadisi maisha ya mtaani ili kuweza kuendana nayo. Sasa hapa inabaki kuwa chozi kwa msomi.Serikali inabidi iingilie kati ili kuweza kuangalia mtaala wa elimu ya kitanzania ili uweze kubadilishwa kuendana na uhalisia wa mtaani.
- Vita kubwa ya wasomi na ambao sio wasomi, sasa hapa ni kutokea vita kati ya walio enda shule na ambao awajaenda. Unajua katika jamii yetu yaa kitanzania watu ambao hawajaenda shule unakuta wanaumia sana kuto kwenda shule. Sasa hapa wanaangalia walio soma wameeda wapi, ukiangalia wengi wao ndo hao hawana hata ajira wapo wanaangaika mtaani. Sasa hao ambao unakuta wanafurahia sasa hii usababisha kuleta huzuni au chozi kwa wasomi.
- Elimu haiwajengi wasomi kufikiria nje ya boksi ,hichi ni kitendo cha mtu kuweza kufikilia vit una kuja na jawabu zuri ili kuweza kutatua matatizo ya mtaani.Kufikiria nje Ya boksi ni msemo mashuhuri wa Mh. Hamisi Kigwangalla.Sasa unakuta elimu yetu haijawaanda wasomi kuweza kuwa hivyo, sasa unakuta wanafundishwa ili wawezo kujibu mtihani basi. Sasa hichi kitendo endapo wakienda mtaani na wakakosa ajira kitawafanya WAKATE TAMAA angali bado umri mdogo. Hi husababisha maumivu makali kwa msomi wakati shida ni mfumo wa elimu sio Rafiki.Hii kauli mbiu kufikiria nje ya boksi ikiwezeshwa, basi wasomi kitawafanya kuona tatizo na kulitatua katika jamii yetu husika.

Upvote
2