Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Mwanamuziki Chris Brown amewasilisha kesi dhidi ya kampuni ya filamu, Warner Bros. Discovery akiidai kampuni hiyo kiasi cha Tshs. Trilioni 1.2, akidai kwamba kampuni hiyo imechapisha taarifa za uongo na zinazomdhalilisha kupitia "Documentary" ya "Chris Brown: A History of Violence"
Katika mashtaka hayo "Breezy" anadaiwa kumdhalilisha kingono Mwanamke mmoja baada kumpa madawa ya kulevya, katika moja ya Sherehe za Sean Combs (P Diddy) mwaka 2020
Aidha, Mwanasheria wa Chris, Levi McCathern amesema "Kesi hii ni kuhusu kulinda ukweli. Licha ya kupewa ushahidi kuwa taarifa hizo si za kweli bado kampuni hiyo iliandaa "documentary" hiyo na kuichapisha kwa makusudi wakifahamu wako kinyume na majukumu yao kama waandishi wa habari."