Chris Mauki umeshindwaje kuelewa nadharia rahisi kiasi hiki?

Chris Mauki umeshindwaje kuelewa nadharia rahisi kiasi hiki?

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Kumekuwa na majadala mkubwa kuhusu kauli ya Dr. Chrisiona Mauki kwamba wanaume wasioacha kitu nyumbani na kila siku wanatoka asubuhi na kurudi jioni ni wasanii. Kauli hii imeibua mjadala mkubwa kwenye jamii na wengine wameanza kumjadili Ndugu Chrisiona badala ya kujadili hoja yake.

Wapo waliomfanyia ‘personal attack’ na kuibua hoja nyingine nje ya hoja yake. Wengine wameibua tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa sababu tu ya kuchukizwa na hoja hiyo.

Mimi si muumini kabisa wa ‘personal attack’ kwahiyo nitajadili zaidi kauli ya Chrisiona kuliko kumjadili yeye mwenyewe binafsi. Hoja ya Dr. Chrisiona SI SAHIHI hata kidogo kwa sababu zifuatazo;

#Mosi Katika maisha kuna kupata na kukosa. Siku hazifanani. Kwahiyo kukosa haimaanishi kwamba wewe ni msanii. Unaweza kukosa leo, kesho, mwezi au hata mwaka mzima lakini huwezi kukosa milele. What matters ni hatua unazochukua kupambana ili utoke hapo ulipo.

Diamond aliwahi kupambana zaidi ya miaka mitano. Anasema kuna wakati alikua anapewa nauli leo kesho anaona aibu kuomba tena, so inamlazimu kutembea kwa miguu. Anatafuta conection za mapromoter, maprodyuza na record label inayoweza kuona kipaji chake. Kwa miaka mitano ya kutoka nyumbani kila siku na kurudi bila kitu Chrisiona angemuita msanii. Lakini mtizame Diamond wa leo.

What matters si hali yako ya sasa bali hatua unazochukua kupambana. Kama umekosa na umekaa tu nyumbani huhangaiki labda Chrisiona anaweza kupata uhalali wa kukuita msanii. Lakini kama umekosa na unapambana kwa nguvu na akili zako wewe si msanii, ni mpambanaji.

Hakuna mwanaume anayetoka nyumbani kwake asubuhi kwenda kushangaa magari barabarani na akarudi jioni. Wote hutoka kwenda kutafuta. Kwahiyo kitendo cha kutoka nyumbani asubuhi na kurudi usiku kilitosha kumfanya Chrisiona awape heshima wanaume hao badala ya kuwaita wasanii.

Kuna wanaume wanatoka nyumbani kwao saa 10 alfajiri wanarudi saa 6 usiku. Analala masaa manne anaamka tena kwenda kupambana kwa ajili ya mke wake na watoto. Kupambana kwa ajili ya kesho yao. Hivi mtu kama huyo hata akikosa unamuitaje msanii? Chrisiona amewakosea sana wanaume.

#Pili Ndugu Chrisiona ni msomi wa kiwango cha 'PhD' katika masuala ya saikolojia na maadili. Bila shaka anaifahamu vizuri nadharia ya ‘Deontological ethics’. Nadharia hii iliyobuniwa na Charlie Broad inatizama zaidi wajibu badala ya matokeo (action should be based on whether it is right or wrong under a series of rules, rather than based on the consequences).
_
Kwa kutumia nadharia hii ni kwamba mwanaume anayetoka nyumbani asubuhi kwenda kuhanagaika na akarudi nyumbani jioni hata kama hajapata kitu ni BORA ZAIDI kuliko yule ambaye hajishughulishi kabisa lakini ana hela. Huyu anayehangaika kuamka asubuhi ana ‘vision’ hata kama hajapata hela ipo siku atatoboa. Lakini yule mwenye hela lakini hajishughulishi kabisa ajiandae kuanguka maana hana vision.

Ndio maaana Wanigeria wana msemo wao maarufu kwamba msichana ukimuacha mwanaume mwenye ‘vision’ ukaolewa na mwenye ‘television’ ipo siku utamuona yule mwanaume mwenye ‘vision’ kupitia television ya mumeo. That's Deontological theory. Sasa Chrisiona alishindwaje kujua theory rahisi namna hii na yeye ana PhD katika area hiyo?

#Tatu kutunza familia ni wajibu wa mwanaume lakini haimfanyi akikosa aitwe msanii. Nabii Elia aliwahi kukosa akaenda kuomba msaada wa chakula kwa mama mjane wa kule Serepta. Akakuta yule mjane amebakiza akiba ya unga kidogo na mafuta nusu chupa kwa ajili ya kula na mwanae then wajiandae kufa maana kulikuwa na baa la njaa na hakukuwa na akiba ya chakula mahali popote.

Lakini Elia alimwambia nipikie mkate kwa unga na mafuta yaliyopo na hutapungukiwa. Yule mama alifanya hivyo, na chupa yake ya mafuta na debe lake la unga havikuwahi kupungua hadi njaa ilipoisha katika nchi ile.

Sasa jiulize ingekuwa leo mwanaume mtu mzima mwenye nguvu zake (kama Elia) aende kuomba chakula kwa mjane angechukuliwaje? Kama hawa wanaohangaika kutoka asubuhi na kurudi usiku wa manane wanaitwa wasanii, je huyu aliyeamua kwenda kuomba akiba ya mjane angeitwaje?

Chrisiona anapaswa akumbuke kuwa kwenye maisha kuna kupata na kukosa, kuna milima na mabonde, kuna mvua na jua. Aliye kivulini asimdharau aliyeko juani na aliye kwenye kilele cha mlima asimdhihaki aliyeko bondeni. Mungu ndiye mpaji wa vyote kulingana na majira na nyakati.

#Nne; Mwanaume hapaswi kukata tamaa wala kuionesha familia yake kuwa ameshindwa. Hilo ni kosa kubwa sana. Baba wa familia yoyote ni mfariji mkuu wa familia yake (Comforter In-Chief). Juzi Julius S. Mtatiro alisema kila mwanaume anaporudi nyumbani, anaenda kuipa matumaini familia yake, hata kama hana senti tano mfukoni. Uwepo wake na tabasamu lake vinainong'oneza familia kwamba "IPO KESHO....KUNA MAISHA BADO....TUNA ULINZI WA KUTOSHA. BADO LIPO TUMAINI."
_
#Tano; Ndugu Chrisiona badala ya kuomba radhi amefanya kosa jingine kwa kudai kwamba ujumbe wake haukueleweka. Huu ni utetezi dhaifu. Kumwambia mtu kwamba hajaelewa ujumbe wako ni kumuita ‘kilaza’ kistaarabu. Yani umetumia ustaarabu kumtukana.

Inawezekanaje mamilioni ya Watanzania wote waliosoma ujumbe wake hakuna aliyemuelewa? Kama ndivyo basi Chrisiona anaweza kuwa mtanzania mwenye akili nyingi sana ambaye anaweza kuandika kitu na nchi nzima isimuelewe. 🤣🤣 So funny. Mi nadhani hana sababu ya kujitetea. Muungwana akivuliwa nguo huchutama. Aombe radhi na si kujitetea kwamba eti hakueleweka!

Malisa GJ
 
Huwezi ukaanzisha vita halafu utegemee adui akuattack unavyotaka wewe na si anavyotaka yeye adui,christina mauki ameanzisha vita na tunaruhusiwa kumuattack kwa namna yoyote tunayoiona inafaa this is all out war bro,tena mimi naenda mbali zaidi namroga kabisa
 
Chris Mauki kama msomi wa PHD, atuonyeshe hiyo PhD inafanya nini kuwakomboa watanzania. Kubeza watu kwa hela za ujanja ujanja wa kupiga mdomo au kuwa MC, sio kigezo kwamba ndio mwanaume unayejua unafanya nini.

Chris Mauki, actions speak louder than words. Show me what you have done so that we put your records straight. Otherwise wewe ni mganga njaa kama waganga njaa wengine. Usitukane wakunga, wakati uzazi bado ungalipo.
 
Msameheni,anajaribu ku repair image/reputation yake...impression management lol,,,,, mama Mauki your husband needs you now more than Ever, you will overcome this, but support each other
 
Aiseee kweli huijui kesho yako,angejua haya usiku kwamba nikiandika hivi kesho patachimbika yani statement yangu ita wavuruga vuruga vichwa mafaza house kutoka kila pembe ya nchi basi asingeamka na kuandika vile,Ona sasa mwanakulitafuta mwana kulipata.
 
Huwezi ukaanzisha vita halafu utegemee adui akuattack unavyotaka wewe na si anavyotaka yeye adui,christina mauki ameanzisha vita na tunaruhusiwa kumuattack kwa namna yoyote tunayoiona inafaa this is all out war bro,tena mimi naenda mbali zaidi namroga kabisa
Hukua na haja ya kutandika mkeka because info uliyojaza ni basic but extended
 
Chrisiona..!! Christina..!! Ni Dr. Chrisostom Mauki, PhD.
 
Huwezi ukaanzisha vita halafu utegemee adui akuattack unavyotaka wewe na si anavyotaka yeye adui,christina mauki ameanzisha vita na tunaruhusiwa kumuattack kwa namna yoyote tunayoiona inafaa this is all out war bro,tena mimi naenda mbali zaidi namroga kabisa
😂😂😂😂😂😂

Hata Magu kasema vita haichagui silaha.
 
Bado mnae!
Eti kasema hatamwattack personally wakati tayari katumia jina la kike kumdhihaki jinsi yake.

Itakuwa kuna ukweli, jambo dogo kama lile kulikuza namna hii ni “tell tale sign” kuwa kawabamba!
 
Back
Top Bottom