Chris Mugalu simuelewi

Mugalu hamna kitu kwa kiwango cha Simba cha sasa.
Nafasi tatu za wazi anapiga nje yeye na golikipa.
Mashindano ya CAF ana goli moja la penati, pamoja na kupikiwa na akina Chama, Miquissone, Kahata, Bwalya nk hana goli la move.
Kisa ati anazuia mabeki wasipande mbele.
Yeye na goli anapiga mpira nje hadi kwenye kibendela.
Kwa wale wapishi hatari wa Simba hata Sapong angefunga magoli mengi tu.
Kwangu sio straika wa kiwango cha kimataifa.
 
Ili timu ishinde kwanza ni lazima iwe na mpira wakati mwingi wa mchezo, sikatai Mugalu anakosa sana magoli lakini uwepo wake unafanya timu pinzani wasiwe wengi golini mwa Simba na hapo ndio unaona ubora wa mabeki wetu.
Kama uliangalia mechi na vita au jaribu kuangalia tena kwa umakini utaona wakati yupo Mugalu linganisha na wakati alipoingia Kagere ni kama Kagere anacheza zaodi kupata magoli na hazuii na hata akipata mpira hakai nayo muda mrefu anaipoteza hivyo beki na viungo watapata kazi kubwa sana wakiwa na Kagere kuliko wakiwa na Mugalu.
Hata kaa ataendelea kukosa magoli usitegemee kuondoka pale ni faida sana kuwa na mugalu.
 
Kazi ya striker ni kufunga, sa unataka afanye nini zaidi wakati kila mechi akiingia anasalimiana na nyavu.
Watu wengine bwana nuksi tu.
Kwa mtazamo wa haraka haraka, kazi ya striker ni kufunga. Lakini kwa mtazamo wa mbali zaidi, striker anaweza kutumika kama mtengeneza space kwa viungo kufunga. Striker anaweza akawa anafanya mikimbio ambayo ikawafanye mabeki wanaomkaba kumchunga zaidi aendapo, na kwa kufanya hivyo akawafanya waache nafasi kwa viungo kufanya yao. Hata hivyo hii haihalalishi kwamba striker akose bao la wazi.
 
Tujikumbushe

1. Platinum vs Simba mugalu alikosa magoli mawili moja alibaki yeye na kipa alikanyaga mpira akaaunguka

2.Simba vs As vita team inapata clear chance nane yeye hana hata shot on target, team ina big chance 6 yeye big chance 3 anakosa zote ,,, Team ina goli nne kwa mechi moja alafu striker hana shot on target


3.Game na Al Merreikh hom and Away anakosa magoli zaidi ya matatu


4.Game na prison inaisha draw kwa sababu ya yeye kutotumia nafasi


5.Game na vita hom anatinga tu mabek hapig shots mpaka anapewa penalty na ole wake angekosa

6.Nasisitiza Da Rosa ni kocha mzuri anajua mpira kuliko sisi amwamin kagere hata kidogo kuliko mugalu
 
Wacha kumtetea galasa Mugalu.
Sawa kaletwa ili akabe huko mbele ndo hata nafasi za wazi za kufunga ashindwe?
Kama kukaba mbele apelekwe basi beki Erasto Nyoni akamiliki mipira pale ndani ya 18.
Straiker maana yake ni kufunga magoli.
Juzi alipotoka na AS Vita tukapata magoli mawili ya haraka. Na angebaki Mugalu wangeweza hata kusawazisha.

Leo ndo nasikia timu inasajiri eti Mshambuliaji Mkabaji.

Kutokana na nafasi alizocheza Mugalu kwenye mechi za CAF ilibidi aongoze kufunga magoli mengi. Lakini wanamzidi hadi viungo.

Kwa hawa viungo mafundi wa Simba namba tisa angesimama Sapong, au Molinga wangefunga magoli mengi sana.
Mugalu kazi yake uwanjani ni kula Big G na kusubiri kuotea.


Kama tungefungwa na AS Vita lawama zote angebeba Mugalu.
 
"Mshambuliaji mkabaji"[emoji23][emoji23]
Hii ndo naisikia kwa wanaomtetea Mugalu.

Kagere kwenye nafasi tatu anafunga goli tatu na nusu"kundandeki dhake"
 
Ila Mugalu jamani pale tumepigwa aisehh.
 
Hiyo point yako ya 6: Kagere ni mzuri na kocha analijua Hilo. Ila bahati mbaya kwa Kagere Ni kuwa hafiti kwenye falsafa ya mpira ya kocha! Kocha anaamini katika multiple tasks for each player depending on circumstances! Kagere ni mzuri kwenye kumalizia tu! Hana msaada katika kuleta Kash Kash kwa mabeki! Hana msaada wakati timu haina mpira! Hawezi kushiriki kikamilifu katika kunyang'anya mpira kutoka timu pinzani! Kwa falsafa ya Gomes hata Rud van Nisterooy aliyekuwa Man U angesugua benchi!!
 
Hivi bado kuna swali kuhusu kwanini Kocha anamchezesha Mugalu instead of Kagere? Nadhani jana umeona! Endelea na uchambuzi wako wa kusadikika.
 
Hivi bado kuna swali kuhusu kwanini Kocha anamchezesha Mugalu instead of Kagere? Nadhani jana umeona! Endelea na uchambuzi wako wa kusadikika.
Bora mkosa magoli mugalu kuliko mpaki Basi iseee..
 
Mugalu.

Mechi mbili, goli mbili.

Ndugu yangu mpira haupo hivyo unavyofikiri.

Quick movements zipi unazosemea? Au ndo bora mradi umechambua?

Leo kapata clear chance moja na goli moja.

Anaweza asiwe mzuri ila sio kama ulivyochambua wewe.
Mkuu nakusalimia
 
Mwabeja,
Right on the money, well said.
 
Apelekwe Namungo kwa mkopo akatafune Big G, chewing gum, jojo na bazooka huko. Kaivunjia hadhi Simba kwa kuwa na mchezaji kama yeye na kututia fedheha sisi mashabiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…