Christianity/Islam tupa mbali na turudi nyumbani

Dini zipi ndugu?mimi mtoa mada ni mkristo tena safi kabisa.sasa neno lako la kusema dini zetu hazina katiba sijui umeliibua wapi.
Kama ni vigumu kunielewa, sasa itakuweje rahisi kwang kukuelewa, ok
Imani zenu zina katiba halali
 
Ni kufanyia modification tu. Hata hizi za wazungu na waarabu zilikua hivyo. Yupo alietakiwa kumtoa kafara mwanawenyewe. Then akapewa kondoo. So ilikua inafanyika. Ukifatilia vizuri hata dini zao zimejengeka kwa misingi ya kafara. Mana hata mungu alitoa mwanae wa pekee ili dhambi zetu zisamehewe
 
Mkuu unajua kuwa wakristo hudai kuwa wao ndiyo wako sahihi na waislamu pia hudai kuwa wako sahihi,sasa nyie mnataka turudi kwenye imani za mababu zetu je huko kuna ukweli gani katika hizo imani ambao utafanya tuone uongo wa hizi dini za kuletewa? maana haiwezekani tufuate hizo imani za mababu kisa tu ndiyo zilikuwa za mababu zetu.
 
Kipindi cha Ibrahim hakukuwa na habari za injili lakini alihesabiwa utii kwa kuwa alifuata taratibu zilizowekwa na alikuwa mwaminifu kwa kile alichoamini. Wazee wetu nao walipata waliyoyaomba kwa sababu walienenda kwa uaminifu kwa kile kidogo walichokijua na MUNGU akaamua kuwaletea mambo sahihi ya kuyafanya ambayo ndiyo mafundisho ya dini zetu. Kuna yaliyoandikwa katika Biblia na Quran tunayaona yakitokea sasa hivyo story ya vitabu vitakatifu si za kutungwa na watu.
 
Naona mzimu wa matambiko umepata afisa masoko mpya.
 
Kuukataa
Ukweli hakufanyi ukweli usiwe ukweli.sikuumba majini na watu ila waniabudu.
 
Imani bwana ukisema uijadiri utajikuta unakufuru bora tupite hivi kila mmoja abaki na anachokiamini, we ukiona ni vema kufanya hivyo hauzuiwi na mtu waweza fanya na hakuna atakaye kufatilia kwa sababu umechagua kuamini hivyo.
 
Tatizo unafananisha Yesu na mifano ya Hovyo kama Ngwanamalundi labda ungekuja na mifano mikubwa ya watu waliofanya makubwa
 

Well ,Sijasema turudi kwenye imani za mababu zetu .I said tuitizame dunia kama ilivyo,because the world begun before Christianity or Islam kwa style hiyo ninaamini tutaimarisha upendo zaidi baina yetu(unconditional love).

I understand that faith is something very personal,na ukiona mtu yeyote anazungumzia imani ya mtu mwingine vibaya whether awe anaabudu chura ,mbwa,mlima ,mungu ...you name it ,basi ujue huyo mtu hana Mental Maturity.
Ukweli ni kwamba sisi ni wa moja,the one looking at you through my eyes ,and the one looking at me through your eyes Is The Same One,but dini itaingilia kati hiyo vision na kusema ,no , you are not the same one ,this is Christian,this is Muslim this is Jew ,we can't be the same .Hilo ndiyo tatizo la dini,"Ego".

Kadhalika pia nimesema imani ni kitu kizuri hasa kwa watu ambao ni open minded,but for small minded ,ni big challenge for sure ,na ukiona sehemu yoyote kuna zogo la dini ujue huyu mtu yupo.Because those people have no room for reasoning ,everything they speak out or spell wanataka izunguke kwenye imani zao,matokeo yake watu wengi sana wanaishi bila ya kuishi,wanakufa bila ya kufa na wanakufa bila ya kuishi ,chanzo ni hizi dini au uelewa wetu kwenye hizi dini.

Like me ,I respect very much imani ya kila mtu whether unaabudu paka au mbwa ,binadam,Jesus Christ ,Allah whatever,frankly I believe we are on the same page,hakuna kati yetu aliyeshukiwa na malaika au mungu na kuambiwa "this is the true path to be" tunajiuliza na kujiambia wenyewe ,henceforth I don't have any reason to judge a person through his or her or its faith .

—Nothing Personal •
 
Mkuu hapo tatizo si dini bali ni watu tu wenyewe,na wanaweza hata kutumia ukabila,utaifa na hata ubaguzi wa rangi Kufanya machafuko yenye kuondoa upendo. Sijajua kwanini ni dini ndiyo upewa lawama kana kwamba zinafundisha kubaguana na kuchukiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…