Dr Guitar tz
JF-Expert Member
- Jan 23, 2018
- 312
- 247
Baada ya kufunga magoli mawili kati ya matatu Christian Ronaldo amekua akipewa sifa nyingi hasa kwa lile goli la tik tak.
Najiuliza nini cha ajabu pale? Mbona ni wengi sana hadi sasa washafunga kwa style ile?
Nilichogundua Cr7 ana Nyota tu ya kupendwa kama ilivyokua kwa David Beckam Na ndio kikubwa kinachompa support kwa watu ingawa nakubali ni mfungaji hodari Mwenye shabaha ya goli, ni shabaha na kariba zilezile za akina Van Persie, Didier, Alex Sanchez Drogba, Suarez, Lewadonsk, Naymar Jr..nk
Mwisho wa Siku unagundua CR7 anasafiria Nyota za kupendwa lakini ni wa kawaida sana.
Kosa moja kubwa walifanyalo wapenzi wa CR7 ni kutaka kumshindanisha na Messi, Kiukweli Messi anakariba na style tofauti na CR7 Kaliba ya Messi kwa sasa waweza kuwaweka group moja na Mohammed Salah, Eden Hazard, hawa sio watu wa front kusubiri kufunga kundi hili wanakua na majukumu mengi zaidi ya nyavu.