Christina Shusho azikwapua milioni 10 za nabii mkuu GeorDavie, amuita mfalme

Machawa wanaongezeka kwenye kila sekta, milioni kumi ndefu, unaweza kumsifia bosi mpaka ujikute unamtukana bahati mbaya bila kujua..
 
Wewe ni Mfalme, wewe ni Baba na si kwamba ni kujifanya wala kujipendekeza ila mimi ni mtoto wako mimi ni binti yako ninasikia Fahari nazungumza maneno haya kwa baba na nasikia nina nguvu ninaposema kitu kwa baba, siyo kitu kingine ni kazi ileile uliyotutia moyo kuendelea ndo hiyo tunaifanya, Baba natamani unipe nguvu"- alisema Christina Shusho.
Christian ana akili na ujanja mzuri sana...
 
Hizo milioni kumi angetoa sadaka ya chakula kwenye msimu wa sikukuu kwa kaya hata 1000 za wale watu masikini na mafukara ambao sikukuu huwa wanapiga pasi ndefu bila kuona mlo wowote angepata fanaka sana.

Mtu ambaye huwa namuelewa ni marehemu mengi kiasi chake kula na walemavu at least mara moja kwa mwaka. Ile ni bonge la sadaka.

Nilifundishwa hii kitu na rafiki yangu m'moja tulikuwa huko mkoani mbeya. Jamaa huwa anahuo utaratibu wa kutoa fungu lake la kumi kwa familia za kipato cha chini.

Tulienda nakumbuka ilikuwa Christmas. Alitenga pesa ya kutosha tukaenda kula sikukuu huko kwa familia ya wanandugu. Aliwanunulia watoto zawadi za Christmas ikiwamo nguo na viatu. Akina mama na wabibi walipata doti za kanga na vitenge na wengine madera na viatu. Baba akapewa zawadi ya suti mpya na viatu. Kisha vikanunuliwa vyakula na vinywaji.

Aisee nilitazama macho ya wana ile familia namna walikuwa wamepata faraja na kujiskia vizuri ile sikukuu. Yaani unaona kabisa kuwa hawa watu wamejisikia vizuri. Aisee yale mapokezi yao nikajiona kama waziri mkuu au rais amekwenda sehemu.

Wakati wa chakula meza ilijaaa vyakula watu walikula na kunywa asiee nikajisikia vizuri sana. Tukaondoka pale nikajifunza jambo la pekee sana tokea siku ile.

Nataka nianze huo utaratibu nitenge at least mara moja kwa mwaka nachagua sikukuu mbili mfano pasaka na Eid.

Natafuta familia ya kipato cha chini ambayo najua kwa life ya hapa mjini ni ngumu wao kuafford chakula kizuri sikukuu. Nikitenga kama laki mbili hivi najua watakula vizuri na watafurahia msosi.

Laki mbili watanunua mchele wa kutosha, nyama ya kutosha na viungo vya kutosha, matunda ya kutosha, soda hapo hawatakosa kreti moja hadi mbili watapata. Namtafuta baba wa familia namwita kando then napanga nae mahitaji then nitakwenda nae sokoni kununua mahitaji kisha tunarejea sote kwake na zawadi za nguo za sikukuu za watoto na mkewe kisha tunashiriki chakula pamoja.

Kuna faraja kubwa sana katika kupata chakula na wale wasiojiweza maana unawapa fursa ya kufurahia na kusheherekea sikukuu kwa kula vizuri na kuwa na faraja.

Tujitoe jamani hii kitu ina baraka kubwa sana kutoka kwa MUNGU.
 
Mkuu zile ni pesa zake unajuaje kama na hayo makundi uliyoyataja hawasaidii? Tusiwe judgemental.

Pili, nakupongeza kwa kutaka kuiga huo utaratibu uliojifunza kupitia rafiki yako, nakuombea ukafanikishe hilo. Tatu, ukiweza jitahidi kumsomeshea maskini(fukara) mtoto wake. Simpendi Nyerere lakini hainifanyi kuwa kipofu juu ya maono au kauli zake nzuri. Alipata kusema, ukitaka kumsaidia maskini msomeshee mtoto wake. Na hili waweza kufanya kwa jamaa zako au watu baki.

Kila la heri.
 
Back
Top Bottom