Chibule
Senior Member
- Sep 25, 2024
- 171
- 230
Chuchu bandia/Pacifier hutumika kama njia ya kumfariji mtoto , kupunguza maumivu, kufanya apate usingizi na pia kumnyamazisha akiwa analia.
MTOTO AANZE LINI KUTUMIA CHUCHU BANDIA ?
Ikiwa wazazi wanapanga kumpa mtoto wao chuchu bandia basi wakati mzuri wa kuanza kutumia chuchu bandia ni baada ya mtoto kuanza kunyonya vizuri, hii inaweza kuchukua wiki kadhaa tangu mtoto alipozaliwa.
KUNA MADHARA GANI YA KUTUMIA CHUCHU BANDIA
Tafiti zimeonesha kwamba matumizi ya chuchu bandia baada ya mtoto kufikisha umri wa miaka miwili mpaka mitatu na zaidi kuna weza kupelekea tatizo la mpangilio mbaya wa meno mfano, meno ya juu kushindwa kukutana na meno ya chini, taya la juu kuwa dogo kuliko la juu , lakini pia meno ya juu na chini kupishana. Hali hii inaweza kuathiri ubora wa maisha ya mtoto kwani inaathiri muonekano lakini pia utafunaji wa chakula.
Hivyo matumizi ya chuchu bandia kwa muda mrefu yanaweza kuleta changamoto katika afya ya kinywa na meno, zitumike kwa muda mfupi ikiwa wazazi wanataka kutumia kwa mtoto.
VITU VYA KUZINGATIA UNAPOTUMIA CHUCHU BANDIA
Epuka kuning'inza chuchu bandia shingoni kwa mtoto, kwani inaweza kumkaba na akashindwa kupumua.
Usitumie chuchu bandia ambayo imeunganishwa na nguo ya mtoto.
Badilisha chuchu bandia kila baada ya miezi miwili kuepuka kuharibika.
Epuka kuipaka asali au sukari, ili kuzuia meno ya mtoto yasioze.