Chuchu: Piga ua lazima Ray atanioa

Chuchu: Piga ua lazima Ray atanioa

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304

LICHA ya hivi karibuni gazeti dada la hili, Risasi kumnukuu mcheza filamu mahiri Vincent Kigosi ‘Ray’ akikana kuwepo kwa mpango wa kumuoa mpenzi wake Chuchu Hans, dada huyo ambaye pia ni msanii wa fani hiyo, ameibuka na kusema piga ua lazima wataoana.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Chuchu alisema hana uhakika kama mpenzi wake huyo alimaanisha kile kilichoandikwa gazetini kwa vile ana mapenzi ya dhati kwake.

“Kiukweli mimi moyo wangu unakataa kama alisema maneno hayo kwa vile ni mtu ambaye namjua ana mapenzi ya dhati kwangu,” alisema.

Mwanadada huyo aliongeza kuwa, anahisi kuna kidudu mtu mwenye nia ya kuleta mtafaruku ndani ya uhusiano wao kwa kuchochea fitina ili mapenzi yao yavurugike.

“Unajua kuwa kuna uwezekano kabisa kuna kidudu mtu ambaye anataka kuleta mtafaruku ili tugombane bila sababu na hilo mimi sikubaliani nalo,” alisema.
 
  • Thanks
Reactions: prs
alaf uyo dada before ya kuwa na ray apikuwa ameolewa..what hapened to her married??
 
Back
Top Bottom