Chui amemfuata mamba majini akamzabua nje na kummaliza

upo sahihi kabisa
 
huyo Mamba wa wapi aiseee.. Kuna siku nilimuona mamba kule Mwanza yani ukubwa wake alijaa ndani ya zile cruiser zenye bodi na bado hapafungi. sasa chui gani anaweza kumnyanyua huyo
 
Hahahah
 
hawa mamba wa kwetu wanaitwa Nile crocodile ni wakubwa sana. Hawawezi kuvuliwa kama hivyo vigators.
 
inabidi tupate elimu ya kutofauytisha hawa wanyama wa jamii moja

huku africa tuna -leopard na cheetah hawa maumbo yao ni madogo hawawezi hata kujaribu kumvamia mamba wa africa (crocodile)

Asia na america kule kuna TIGER na JAGUAR haya madude yana maumbo makubwa kama huyu simba wa huku kwetu na hata madoa yake yanakuwa makubwa sana(TIGER) jagua yy wapo wenye madoa na weusi tupu

huku africa tuna MAMBA (crocodile) huyu hukua kufikia na hata kupita urefu wa futi kumi na uzito hadi wa tani 1 na nusu hili dude ni balaa hasa likiwa kwenye maji lina uwezo wa kubeba mnyama mwenye kilo hata 400 na kumrusha majini kama karatasi (chui mwenye kilo 60 ataweza kweli kulibeba hili dude)

kule america kuna aligators na Caimans hawa ni jamii ya mamba ila tofauti yao ni kwamba hawa ni wadogo sana kimaumbo na hata ikicheki sura zao mamba imekaa V ila wao sura zao zimekaa U shape... mamba hawezi kuficha meno yake ila hawa caimans na aligators wanaweza kuyaficha meno yao na yasionekane..

conclusion.... yule kwenye ile makala alikuwa ni TIGER a grown up Tiger akimkamata a young aligator/caiman

Naomba kuwasilisha
 
Kuna Jaguar wa America kusini huwa wanakula mamba kama kawaida, haijalishi mamba yupo majini au nchi kavu, mamba akiwaona tu huanza kutimua mbio kama wanaume wa dar wanavyokimbia wakimwona nyoka
Ahahaaa kuna watu mna matatizo sana kwahiyo wanaume wa dar wanaogopa sana nyoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…