Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Utamsikia mtu anasema "hakika namchukia mtu fulani yaani sitaki hata kumwona "
Huyu hajui kuwa anajidhuru yeye mwenyewe,,, kwanza anaishi na nguvu hasi ambazo zina mwangamiza na kumtafuna yeye binafsi.
Hivi umeshawi kuwaona watu ambao wana roho ya korosho au kwa maana nyingine roho mbaya, hawa mara nyingi huwa wamenyauka kutokana na roho mbaya,, si kila mtu mwembamba ana roho mbaya hapana, ila wembamba wa watu hawa huwa tofauti sana kwakuwa wanatafunwa na nguvu hasi nyingi hivyo hukosa hata nuru.
Wewe unayeendekeza chuki tambua unajidhuru wewe mwenyewe kwakuwa kila utapokutana na yule unaye mchukia basi chuki inadhidi na kuzalisha kemikali mwilini mwako ambazo zinakudhuru wewe mwenyewe, na istoshe unakosa raha na amani moyoni mwako.
Na kibaya zaidi huyo unayemchukia haathiriki kama wewe kwakuwa yeye amekubali kuwa unamchukia na anaendelea na maisha yake,,, unabaki wewe unajishughulisha kwa kutaka kumuona anaharibikiwa, anaanguka na kupata madhira mbali mbali na kuanguamia,,, usichojuwa baraka zinatoka kwa Mwenyezi Mungu na humbariki amtakaye bila hesabu
Jifunze kuishi bila chuki hata vitabu vya dini vinasisitiza sana kusameheana na kugawa love kwa binadamu wenzetu.
Kwani asiye msamehe mwanadamu mwenzake hata huyo aliye juu zaidi na ambaye ni mkuu hatokusame pia.
Upendo ni nuru, upendo ni amani, upendo ni furaha, kuwa huru kwa kuepukana na chuki,,, siku zote chagua tabasamu.
Ni hayo tu!