Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Tangu awamu hii iingie madarakani kuna dalili za ukweli kuwa chuki inazidi kujengeka sana miongoni mwa jamii. Nina ndugu yangu upinzani lakini amekuwa na kinyongo sana nami (ingawa haoneshi) kwa namna uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulivyoendeshwa. Anazungumza huko, watu wanasikia, wananiambia lakini mimi najifanya kutosikia na napinga kuwa ni udhaifu wake tu.
Nitaendelea kuangalia kila nyanja ambayo inaonesha kuleta dalili za chuki miongoni mwetu lkn leo nitazungumzia kidogo kuhusu tasnia ya Sheria. Kwa kifupi uongozi huu unaonekana kutowapenda Wanasheria - hasa wanaofanya kazi zao binafsi.
Wanasheria waliomo mfumoni wanajaribu kuwabinya wale wa binafsi. Mbinyo huo lakini pia unagusa hata wale waliomo mfumoni, kwa sababu nao wanaambiwa wameanzishiwa mfumo wao wa kusimamia mambo yao kwa kuanzishiwa chama chao, sijui Public Service Bar Association.
Ukiangalia utaratibu wa uanzishwaji wa Chama chenyewe ni maigizo tu. Hamna uratibu, hamna bajeti, hamna umakini na umaanani ilimradi tu waonekane wapo wapingane na wenzao wa binafsi.
Ukiangalia sababu kubwa ya kuanzisha Chama hicho ni kwa ajili ya kuifanya TLS kuwa nyonge. Lakini sasa, cha ajabu ni hicho Chama chenyewe kabla hata hakijaanza rasmi kinaonesha wazi kutokuwa na manufaa yeyote kwa wanachama wake. Inafikirika kuwa chuki inajengwa kati ya Wanasheria wafanyao kazi Serikalini na wale wa binafsi lakini uhalisia sio hivyo chuki inayojengwa ni kati ya wanasheria wa Serikali na Serikali yenyewe. Nani hajui awamu hii inavyokandamiza watumishi wa umma. Nakiri wapo wasio wasafi lkn wapo wasafi wengi pia wamekandamizwa.
Eti Mwanasheria wa Serikali asifanye kazi cha kujiingizia kipato binafsi, sijui hapo imekaaje kwa sababu hata mshahara wenyewe una harufu ya JK. Allowances ndiyo zimeondolewa, safari za kupiga na manati, huduma ya NHIF imekuwa ya bando, halafu unataka wakashinde kesi! Ajabu sana!
Ukweli wanaogopa tu kusema ili wasipotezwe na kubambikiwa makesi ya utakatishaji fedha ili sisi wenye ndugu wanaofanya kazi Serikalini tunayasikia vizuri malalamiko yao tunapokuwa nyumbani sebuleni na tumefunga milango tusisikiwe au kudukuliwa maongezi yetu iwapo tutayaongea mitandaoni.
Kule TLS kuna wakina Werema na wakina Hosea (yule Mkuu wa PCCCB) ambao walikuwa wanasheria wa Serikali na wanafurahia mijadla ya TLS. Leo wakina Kilangi wanatengeneza mazingira magumu kufanya kazi wakitoka Serikalini na wanajijengea chuki kwa wenzao bila kujua. Muswada wa Sheria ya TLS ulivyokaa kwa sasa ni kitanzi kwa tasnia, si wa binafsi wala wa Serikali wote humo humo.
Nasikia hivi karibuni wale wa Serikali waliambiwa watakuwa na mihuri yao, mpaka leo haijulikani hiyo mihuri ni kweli itakuwepo? Chuki ya ndani kwa ndani inaendelea kumea. Wanasheria wanalalamika tu, si wa Serikalini si wa binafsi. Wa Serikalini mishahara haipandi halafu wanategemewa wafanye kazi kwa uzalendo, uadilifu na kwa unyenyekevu. Wanabanwa wasiungane na wenzao wa TLS, chuki inakolezwa.
Sasa angalia kwenye utungaji wa Sheria za nchi. Sheria zinatungwa za kiimla, imesahaulika kuwa hizo hizo zitakuja kuwabana watawala hao hao watakapokumbwa na kadhia wakitoka madarakani. Angalia Zambia, Israel na kwingineko ambako viongozi wao wa juu waliopita waliwahi kufikishwa mahakamani. Ni suala la muda tu. Zuia demokrasia leo miaka kadhaa ijayo mwanao pia ataikosa demokrasia hiyo kama unavyowanyima wenzio.
Lazimisha wenzio kukiri makosa ambayo hawajayafanya leo, na mwanao au wewe mwenyewe utakuja kulazimishwa kukiri makosa kama uwafanyiavyo wenzio. Ni suala la muda tu iwapo chuki inaenezwa. Watu wana hali mbaya, ukandamizwaji wa wazi lakini utawala unasonga tu mbele.
Leo naishia hapa basi tuendelee tu kuimarisha chuki miongoni mwetu. Tutavuna tunachopanda!