Chuki nichukie roho yangu niachie!

Chuki nichukie roho yangu niachie!

Bwana kaduga

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
863
Reaction score
1,812
Habari zenu ndugu wenyenchi?

Naam! Leo tena katika mada,
Ndugu wenyenchi safari ya mada ya Leo inaanzia hapa:

Mwaka 2010 nikiwa katika kazi ya ufundi wangu wa rangi kipindi hicho ndio nilikua nikifundishwa na fundi wangu mkuu, hivo tulikua tukifanya kazi ktk nyumba furani hivi na boss wetu alikua ni mtumishi wa serikalini huku akiwa na msimamizi.

Basi boss alipo kuwa akija kukagua na akinikuta katika ubora wangu wa kazi, alikua akipendezwa sana na kazi zangu hivo alitokea kunikubali sana, huku akionyesha kwa mafundi wenzangu pamoja na fundi wangu mkuu.
Kumbe wakati hayo yote yakitendeka wenzangu walikuwa wakiangalia kwa jicho LA hiana, boss alifika mbali ktk kunikubali hadi ikafikia kipindi ananichukua tunaenda nae kununua material na hadi kwake tunafika.

Kumbe yote haya yakitendeka wenzangu walikua hawapendi hususani fundi wangu mkuu, ilikuja kuwauma zaidi walipo sikia kuwa boss anataka anipeleke dar nikawe msimamizi wake wa baazi ya investment zilizopo huko, Basi alichokifanya fundi mkuu in kwenda kuongea na boss, kwa mujibu wa maelezo ya bosi alio niambia nikuwa;

Aliniita Boss; "Kaduga"
Mimi; naam boss
Boss; nilikuamini sana tena sana hadi nikafikia uamuzi wa kutaka kukupeleka kule dar kama nilivo kuambia.
Mimi; vipi bosi mbona kama unaonesha kunakitu nimekukosea?
Boss; hapana Kaduga hujanikosea ila kwa mujibu wa maelezo ya fundi wako zoezi inabidi tulisitishe.

Mimi; ni maelezo gani hayo aliyo kupatia?
Boss; ameniambia kuwa wewe ulisha kabidhiwa duka kubwaa na mjomba wako lakini ulishindwa kulisimamia vizuri pia ulikuwa umepewa stationary lakini ukashindwa kuisimamia, ndipo ukawa mtaani hadi mlipo kutana na fundi wako ndio ukawa ktk fani hii.
Kwa hivo mdogo wangu Kaduga samahani sito weza kukuamini tena maana unaweza kuwa ni chanzo cha Mimi kufirisika.

Mimi; boss unayo niambia ni kweli umeambiwa na fundi??? Daahh!
.................

Kwa hivo tayari nikawa nimeharibiwa dili huku maneno mengi yasio sahihi wakiendelea nikandia, hili nitukio langu binafsi ila kuna mengi nilio yaona kwa ndugu jamaa na marafiki, jinsi binadamu tulivo na chuki na hii chuki huja kwa njia mbalimbali.

Mfano juzi kati hapa imetokea hapa hapa jamiiforum ingawa watu hatujuani lakini bado chuki tunaleteana, kiumbe wa mungu GentaMycen tumeona wakimletea chuki ya waziwazi tokea pale walipo anzisha chuki zao RAIA hadi sasa simuoni hapa najitahidi kumtafuta lakini simuoni na chanzo cha kutoonekana ni hizihizi chuki tulizo nazo za kumchukia MTU.

Sawa lakini kwa kuwa ndio tumeumbwa hivo haina budi kuwa hivo maana huwezi kufosi wote tuwe sawa ila tunapo chukiana basi roho zetu tuachiane sio tusubiliane vichochoroni.

JAMIIFORUMS GREAT
THINKERS.
 
Samahani bwana kaduga, wewe ni fundi rangi unafanya kazi sadoline au mpaka rangi? Maana nakushangaeni wapaka rangi mnapojiita mafundi rangi kumbe mafundi rangi wapo kiwandani wanatengeneza rangi. HII NI NJE YA MADA
 
Mimi nmeshapitia mambo mengi sana ya chuki katika lkn cha muhimu ni kusamehe tu na kuendelea na maisha bila hivyo utaumiza moyo wako tu
 
Samahani bwana kaduga, wewe ni fundi rangi unafanya kazi sadoline au mpaka rangi? Maana nakushangaeni wapaka rangi mnapojiita mafundi rangi kumbe mafundi rangi wapo kiwandani wanatengeneza rangi. HII NI NJE YA MADA
hahaaaa"
 
Back
Top Bottom