Chuki, unafiki na uzushi maofisini tiba yake ni nini?

Chuki, unafiki na uzushi maofisini tiba yake ni nini?

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Hili jambo la Maofisini kuwa tabia za ajabu ajabu zinanikera sana, kuna ofisi yaani kufanya kazi inakuwa ni ngumu na changamoto kwa sababu ya chuki na fitina za hapa na pale.

Na kitu kibaya utashangaa hata boss anaekuzidi mshahara na cheo anakujengea chuki kubwa dhidi yako.

Huku Maofisini nimeona haifai kuzoeana na watu Wala kuwa na urafiki na mtu maana hiyo ndo silaha watatumia kukuangamiza, huku Maofisini inabidi wafanyakazi wenzako wasijue mambo yako nje ya ofisi, nenda fanya kazi ondoka.

Chuki na stress za maofisini zimeletea watu wengi magonjwa na msongo wa mawazo.
 
Binadamu ameumbwa ni mbinafsi sana.Sasa,ule ubinafsi huujaza moyo wake na kumdanganya anatakiwa amiliki vyote.

Yaani vitu vyote bila gharama na kuwa mmliki wa watu na vitu ..Bila kujua kwamba ameumbwa awe na wivu ili atafute vyake kwa uhalali bila kuacha ugomvi na nongwa kwa kutulia katika milki na mipaka yake kwa heshima.

Ukikaa na kuyajua hayo unapaswa "uufundishe" moyo wako kuvumilia na kuyachukulia mambo yalivyo.Ishi kwa akili,heshima,ujasiri ila usiogopeogope hadi ukajiogopesha nafsi yako.
 
Abby Newton alishajaribu kutoa mwongozo
 
hili jambo la Maofisini kuwa tabia za ajabu ajabu zinanikera sana, Kuna ofisi yaani kufanya kazi inakuwa ni ngumu na changamoto Kwa sababu ya chuki na fitina za hapa na pale...
Dawa yake ni kuwa na boundaries tu.
Ila fitna haikosi mahala kokote kwenye riziki.

Kila mtu hapo anaangalia ugali wake, hivyo maeneo hayo kila mtu aishi kwa utu ila akumbuke hiyo ni sehemu ya riziki na aweke mipaka (boundaries) na watu, asiwe na mazoea ya kupitiliza na wenzake mpaka yakawa ndio mwanzo wa negative energies na njama kumfikia na kumuangusha
 
Kuna mtu alipata msiba watumishi wenzake walifika msibani baada ya msiba alipewa Uhamisho.
Unakuta boss anakuzidi pesa wewe unamzidi maendeleo hapo chuki ni lzm
 
Kuna mtu alipata msiba watumishi wenzake walifika msibani baada ya msiba alipewa Uhamisho.
Unakuta boss anakuzidi pesa wewe unamzidi maendeleo hapo chuki ni lzm
Kwa hiyo walivyoenda kwake na kukuta ana maendeleo kuwazidi wakajichukiza?Na hapo ina maana boss anakuzidi mshahara ila hana akili zifanyazo kazi itakiwavyo muungwana awe.😂😂😂😂
 
Kwa hiyo walivyoenda kwake na kukuta ana maendeleo kumzidi wakajichukiza?😂😂😂😂
Yeah
Qq1²wwwwwwww
Kwa hiyo walivyoenda kwake na kukuta ana maendeleo kuwazidi wakajichukiza?Na hapo ina maana boss anakuzidi mshahara ila hana akili zifanyazo kazi itakiwavyo muungwana awe.😂😂😂😂
Yes, unategemea nini kama mtu unajipenda unapenda ukae pa zuri.We upo bize kuzurura kwenye hardware's wao wapo bize kuzurura kwenye bar zenye pisi kali lazima wakuchukie
 
Yeah
Qq1²wwwwwwww
Yes, unategemea nini kama mtu unajipenda unapenda ukae pa zuri.We upo bize kuzurura kwenye hardware's wao wapo bize kuzurura kwenye bar zenye pisi kali lazima wakuchukie
Wakati mmoja anarudi jioni nyumbani na mfuko wa saruji,kuna mwamba anabugia mfuko wake wa saruji uliobadilishwa katika muundo wa bia.😂😂😂
 
Akili za kitoto tena?Hadi amegundua hizo tabia ina maana anajitambua na ndiyo maana anasaka njia mbadala za kupambana na changamoto.Isingekuwa hivyo angejinyonga kwa sonona.
Chuki anazitafuta kazini kapelekwa na uwezo wake sio connection wala uchawa kwa nn achukiwe, kuwa introvert hao anao watongoza ndo chanzo cha chuki ,urafiki wa kijinga unataka kila mtu ujuane nae ya nn ?watu wakikijua tu kwenu hata kama una kamjengo cha mkopo basi ni vita
 
Hili jambo la Maofisini kuwa tabia za ajabu ajabu zinanikera sana, kuna ofisi yaani kufanya kazi inakuwa ni ngumu na changamoto kwa sababu ya chuki na fitina za hapa na pale.

Na kitu kibaya utashangaa hata boss anaekuzidi mshahara na cheo anakujengea chuki kubwa dhidi yako. Huku Maofisini nimeona haifai kuzoeana na watu Wala kuwa na urafiki na mtu maana hiyo ndo silaha watatumia kukuangamiza, huku Maofisini inabidi wafanyakazi wenzako wasijue mambo yako nje ya ofisi, nenda fanya kazi ondoka.

Chuki na stress za maofisini zimeletea watu wengi magonjwa na msongo wa mawazo.
Umesahau na ushirikina. Maofisini Kuna michezo michafu sana ya kuchafuana au kupigana mikosi
 
Back
Top Bottom