Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I said "Being born again " in churches they many church goers not true worshippers . Your working place must be influenced by the kingdom of GodHata huko kwenye nyumba za ibada fitna zipo, kwa wale ambao rizki zao zimefungamana na kuhudumu kwenye maeneo hayo, ambaye unaenda kuabudu tu huwezi ona ila wafanyao kazi ya kuendesha maisha kupitia nyumba za ibada wanajua kuwa fitna zipo humo kama mahala kwengine kokote
Wakigundua kwamba hauna njaa ila unalia njaa, chuki itakuwa mara elfu 1, mana watakuwa wanaona unawasanifu ukiwa unalia njaa.Sijui utauchukuliaje ushauri huu ila ukitaka kufanikiwa fanya hivii;
Hakikisha ukiwa ofisini unatangaza njaa na shida mda wotee yaani wewe ni kulalamika kuwa huna kodi mara mshahara umeisha tarehe 5, ukienda lunch na wenzako hakikisha unalalamika na kujisemesha wakati wa kulipa muhimu hakikisha hakuna mbuzi yeyote hapo ofisini anafahamu kwako kama umejenga na iwapo imelazimika apajue basi wew waeleze kuwa hapo ni kwa shemeji yako.
Hii ni kwa sababu watu wengi maofisini hawapendi kusikia raha zako bali shida zako pekee, so ukiwaeleza shida tu watapata amani mioyoni mwao hivyo kukaa vikao vya kukupuuza.
Uko sahihi sana, Mimi nalijua hili kwa undani wake, tena RC kunanuka kwani ni kimya kimya! Kama shwari kumbe dhoruba kali sana!!!Hata huko kwenye nyumba za ibada fitna zipo, kwa wale ambao rizki zao zimefungamana na kuhudumu kwenye maeneo hayo, ambaye unaenda kuabudu tu huwezi ona ila wafanyao kazi ya kuendesha maisha kupitia nyumba za ibada wanajua kuwa fitna zipo humo kama mahala kwengine kokote
Sipo hivyo unavyosemainaonekana wew ndio una matatizo hapo kazin kwenu, huwez kuona wenzako wana chuki unafki na uzushi halafu wewe uwe perfect, maana yake wew ni mchawi mfitini na unapenda umbea kufuatilia maisha ya watu... Fanyakazi maliza rudi nyumban acha kufuatilia yasiyokuhusu... Ila pole najua tatzo hulipwi vzuri
Dawa ya matatizo hayo ni kumuomba Mungu akuepushe nao.Hili jambo la Maofisini kuwa tabia za ajabu ajabu zinanikera sana, kuna ofisi yaani kufanya kazi inakuwa ni ngumu na changamoto kwa sababu ya chuki na fitina za hapa na pale.
Na kitu kibaya utashangaa hata boss anaekuzidi mshahara na cheo anakujengea chuki kubwa dhidi yako.
Huku Maofisini nimeona haifai kuzoeana na watu Wala kuwa na urafiki na mtu maana hiyo ndo silaha watatumia kukuangamiza, huku Maofisini inabidi wafanyakazi wenzako wasijue mambo yako nje ya ofisi, nenda fanya kazi ondoka.
Chuki na stress za maofisini zimeletea watu wengi magonjwa na msongo wa mawazo.