KERO Chuki wanazotengeneza Mgambo wa Ilala ipo siku watayaona matunda yake

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni dereva Bajaj kupitia Taksi Mtandao, juzi nilimfuata mteja maeneo ya Msimbazi A kumpeleka Fire, pale Sheli (kituo cha mafuta).

Nalipofika nilipark pembeni nikawasha double hazard, wakaja Mgambo wa Jiji wakaniambia ni wrong parking tukabishana pale, wakawa wanataka twende Lumumba au niwape 20,000 nikagoma vyote.

Hivyo, basi tunaomba msaada kukemea hili, wanatengeneza chuki kwa jamii na serikali.

Nakumbuka wakati tupo NIT nilisoma Sheria za Maegezo, hivyo cha ajabu kitendo cha kushusha na kupakia mteja tena pembezoni mwa barabara kitendo cha dakika kadhaa tayari ni wrong parking.

Hivi Ilala imekuwa na sheria ngumu kiasi kile, na kingine wale waliopewa mamlaka, basi wanatumia kuonea vijana, chuki wanazotengeneza ipo siku matunda yake yataibuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…